The House of Favourite Newspapers

Tigo kuwawezesha wasichana kujiendeleza kiteknolojia

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam ambap okampuni ya Tigo ilitoa msaada kwa ajili ya kuwajengea uwezo wasichana na wanawake kwenye sekta y aHabari na  Mawasiliano. Wa kwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Imni Patterson, anayefuatia ni mwanzilisi wa taasisi ya Apps and Girls, Caroline Ekyariisma. 
Halima Okash kutoka Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii cha Tigo akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani) juu ya ufadhili wa kampuni ya Tigo kwa mradi wa‘TECH IS FEMALE’ unaolenga kuwajengea wanawake na wasichana uwezo kwenye Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Wa kwanza kulia ni mwanzilishi wa taasisi ya Apps and Girls, Caroline Ekyariisma, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Simon Karikari, akipata maelezo kutoka kwa wasichana wanaojengewa uwezo kwenye sekta ya Teknolojia ya Habari na  Mawasiliano muda mfupi baada ya uzinduzi wa mradi wa‘TECH IS FEMALE’ ambao Tigo imeufadhili katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasichana wanaojengewa uwezo kwenye sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na taasisi ya Apps and Girls wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafadhili wao ikiwamo Kampuni ya Tigo.

 

 

Ijumaa, Machi 8, 2019  Kampuni ya mawasiliano ya Tigo, imeelezea dhamira yake ya kusaidia kuwajengea uwezo wasichana na wanawake kwa ujumla kwenye eneo la teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kupitia taasisi ya hapa nchini inayojulikana kama Apps and Girls.

 

Akizungumza mbele ya wasichana wenye ndoto za kuwa wajasiriamali kwenye sekta ya TEHAMA wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘TECH IS FEMALE’, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Bw. Simon Karikari alisema, Tigo inatambua mchango wa wasichana na wanawake kwenye maendeleo na kuelezea utayari wa kampuni hiyo kuunga mkono jitihada za kuwawezesha kutoa mchango wao.

 

“Uwezeshaji unaofanywa na Tigo kwa wasichana na wanawake, unalenga kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kigunduzi kwenye TEHAMA kwa makundi ya wasichana waliofanyiwa mchujo na ambao watapewa mafunzo maalum kabla ya kuwekwa chini ya uangalizi maalum wakati wakifanya miradi waliobuni wenyewe ya kibunifu,” alisema Karikari.

 

Karikari aliongeza kuwa, mradi huo wa ‘TECH IS FEMALE’ unalenga kutoa fursa sawa kwa wasichana wote wenye umri kati ya miaka 14 na 24 (wanafunzi na sio wanafunzi) nchini Tanzania ili kuwawezesha kiuchumi na kidijitali, waweze kuwa vinara katika ulimwengu huu wa kidijitali unaokwenda kwa kasi kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia ya kila siku.

 

Kwa upande wake, Muasisi wa Apps and Girls, Caroline Ekyariisma, alisema kwamba kampeni hiyo itakuwa ni ya mwaka mzima. “Lengo letu ni kutoa mafunzo ya kutengeneza programu kwa wasichana katika shule 61 za sekondari zilizo chini ya mpango wa Tigo E-schools nchi nzima.

 

Mpango huu pia utahusisha makundi ya wasichana ambao hawapo mashuleni, hivyo wasichana ambao sio wanafunzi pia watapata fursa sawa ya kushiriki na kunufaika,” alisema.

“Tunapenda pia kutoa shukrani zetu kwa Mpango wa Uvumbuzi kutoka Afrika ya Kusini (SAIS2) pamoja na Mfuko wa Uvumbuzi kwa ushirikiano na uwekezaji wao katika kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kupata ujuzi kwenye TEHAMA,” alishukuru Ekyarisiima.

 

Mchakato wa kuwapata wasichana watakaoshiriki katika mradi huu utafanyika nchi nzima na utakuwa na mchujo mkali ambapo wasichana 30 bora ndiyo watakao fuzu. Wasichana hawa ambao watakuwa mchanganyiko wa wanafunzi na sio wanafunzi, wataingizwa katika mpango maalumu ya mafunzo na uangalizi. Wengine watafanya mafunzo kwa vitendo katika idara ya TEHAMA ya Tigo kwa ajili ya kujiendeleza na kujifunza zaidi, huku wengine wakishughulika na miradi mengine. Wakati huo huo tutakuwa tunawajengea uwezo na kuwasaidia kupata kazi na
kuwapatia mazingira bora ya wao kujiajiri,” alifafanua Ekyarisiima.

 

“Tigo inaendelea kutengeneza kizazi cha kidjitali. Ushirikiano wetu na Apps and Girls ni kuwekeza katika vijana wanawake ambao wanaonesha dalili nzuri za kuwa wajasiriamali, wavumbuzi, viongozi na mifano mizuri katika sekta ya teknolojia nchini Tanzania na Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tunaamini kwamba katika siku za usoni ‘TECH IS FEMALE’ na tunaahidi kujitolea kupunguza tofauti za kijinsia kwenye sekta ya kidijitali nchini Tanzania,” alisisitizaKarikari.

 

Kwa miaka kadhaa sasa Tigo imekuwa ikishirikiana na kampuni ya Apps and Girls ili kuweza kupunguza tofauti ya kijinsia katika sekta ya kidijitali hususani katika eneo la Dar es Salaam. Ushirikiano huu kwa Apps and Girls umefanikiwa kuwafikia wasichana zaidi ya 3000 mashuleni na kwenye maeneo mengine ya jamii nje ya shule, na kuwezesha kuzaliwa kwa wajasiriamali, wavumbuzi, vioo kwa jamii na viongozi katika sekta ya teknolojia ambao wanaleta mabadiliko chanya katika nchi ya Tanzania.

Comments are closed.