The House of Favourite Newspapers

Tigo na Benki ya Azania Waja Huduma Mikopo ya Jibustishe Kwa Wateja Wao

0
Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa huduma hiyo.

 

 

KAMPUNI ya mtandao wa siku za mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Benki ya Azania wamezindua huduma ya Jibustishe ambapo watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa kupitia mtandao wa Tigo wataweza kukopa fedha katika huduma hiyo wanapokuwa hawana pesa kwenye salio la Tigo Pesa.

 

Akizungumza kwenye uzinduzi huo wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema;

Wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo.

 

 

“Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutufikisha hapa tulipo pamoja na wenzetu wa Benki ya Azania kwa kuamua kuungana nasi na sote kwa pamoja kuanzisha huduma mpya ya Jibustishe kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha akiwaelekeza kwa vitendo wageni waalikwa jinsi ya kujiunga na huduma hiyo.

 

 

“Hii ni huduma inayomuwezesha mteja kuweza kufanya miamala wakati hana salio kwenye akaunti yake ya Tigo Pesa kwa kifupi hii ni huduma ya mkopo.” Amesema Angelica.

Akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kujiunga na huduma hiyo, Angelica amesema unachotakiwa ni kuanza na kujisajili kupitia menyu ya Tigo Pesa au App ya Tigo Pesa yaani unapiga *150*01# kisha chagua namba 7 huduma za kifedha, kisha chagua namba 4 huduma za mikono na malizia kwa kuchagua namba 2 ambayo itakupeleka kwenye huduma ya Jibustishe.

Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha (kulia) na Meneja Mwandamizi wa Fedha Masoko na Mitaji, wa Benki ya Azania, Bwana Rukwaro Semkoro wakipeana mikono kwa pongezi baada ya uzinduzi huo.

 

 

Kwa upande wa Benki ya Azania, Meneja Mwandamizi wa Fedha Masoko na Mitaji, Bwana Rukwaro Semkoro amesema huduma ya Jibustishe itawawezesha wateja wa Tigo Pesa kuweza kukopa mikopo ya muda mfupi ili waweze kukamilisha mahitaji yao mbalimbali. Bwana Rukwaro ameendelea kusema;

“Huduma hii kwa kuanzia itakuwa ni kwa wateja ambao wameshatumia huduma ya Tigo Pesa kwa zaidi ya miezi sita hivyo basi wateja wote wa Tigo mnaruhusiwa kuanza kupata huduma hiyo kuanza sasa baada tu ya uzinduzi huu”.

“Matarajio yetu ni kwamba wengi watatumia huduma hii ili kujikwamua kwenye shughuli zao mbalimbali”. Alimaliza kusema Rukwaro.

Leave A Reply