Tigo Tanzania kushirikiana na East African Got Talent (EAGT)

Mtaalamu wa Kidigitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)katika uzinduzi wa promosheni ya EAGT Trivia ambayo ni sehermu ya matumizi ya Kidigitali ya Tigo katika mkakati wake katika uzoefu kutoa huduma bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa wateja wa Tigo.Kulia kwake ni Mratibu wa mradi wa EAGT Redemptus Caesar,

 

Dar es Salaam. Septemba 17, 2019. Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imetangaza rasmi kuingia ushirikiano na kampuni maarufu ya kusaka vipaji ‘Got Talent’ na Clouds Media International. Maonyesho hayo kwa jina Kampuni maarufu kama ‘East African Got talent’ imedhamiria kukuza vipaji Afrika Masharika kwa upande wa kucheza na kuimba.

Ushirikiano huu unakwenda sambamba na uzinduzi wa promosheni ya EAGT Trivia ambayo ni sehermu ya matumizi ya Kidigitali ya Tigo katika mkakati wake katika uzoefu kutoa huduma bora na zenye viwango vya hali ya juu kwa wateja wa Tigo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mtaalamu wa Kidigitali kutoka Tigo, Ikunda Ngowi, alisema, mkakati huo wa Tigo umekuja kwa wakati muafaka ambapo tayari wamekwishapata kasi, na kuwa kazi iliyopo  ni kuhakikisha wanafika ukanda mzima

“Kama kampuni ya mapinduzi ya kidigitali, kila mara tunaagalia majukwaa na mianya ambapo tunaweza kuunganisha wateja wetu pamoja. promosheni ya EAGT Trivia itatoa fursa sawa kwa wateja wetu kusimama pamoja kujishindia zawadfi za pesa taslimu na kwwenda kushuhudia onesha la moja kwa moja nchini Kenya,”

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi wa EAGT Redemptus Caesar, Redemptus Caesar, alisema “Tuna furaha kuugana pamoja na Tigo mojawapo ya kampuni kubwa zinazoongoza kwa mawasiliano nchini Tanzania- Tunatarajia kuweka msingi thabiti kwa vijana wa Tanzania kuonesha vipaji vyao duniani,”

Hata hivyo Ngowi alifafanua kuwa wateja wa Tigo watakiwa kuchamgamkia fursa hiyo, huko akisisitiza kila mteja kujitokeza kushiriki.

“Kupitia promosheni hii ya EAGT Trivia, wateja wa Tigo watakuwa na nafasi ya kushinda zawadi za pesa taslimu hadi kufikia sh. mil. 7. Mbali na hiyo, wateja arobaini (40) watajishindia safari kwenda Kenya kutizama onesho.

Wateja wa Tigo wanaweza kujiunga na Trivia kwa kutuma neno ‘TALENT’ ’kwenda 5572’ au kutembelea http://tigoquizkitaa.co.tz. Baada ya kujiunga mteja atakuwa akijibu maswali yanayohusiana na EAGT, ili kujishindia zawadi mbalimbali za shindano hilo.

Wateja wa Tigo pia wanaweza kutizama onesho hilo kupitia intaneti ya Tigo 4G+ kupitia kifurushi cha YouTube chenye thamani ya Sh 1000 kwa GB1 kupitia menu yetu rahisi *147* 00#

 


Loading...

Toa comment