The House of Favourite Newspapers

Tigo Washinda Tuzo Ya Kuzingatia Usalama Na Afya Kazini Kwa Mara Nyingine

0

Morogoro: Kampuni Namba moja nchini kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali Tigo Tanzania, Leo Aprili 28 , 2023 imetangazwa ( Kwa mara ya pili sasa ) kama kampuni ya Mawasiliano ya simu namba moja nchini inayozingatia Usalama na Afya mahala pa kazi.

Tigo wamekabidhiwa Tuzo hiyo na Mhe. Prof. Joyce Ndalichako Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) katika Maonesho ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi ambayo yameandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi ( OSHA ) ambayo kwa mwaka huu yamefanyika mkoani Morogoro yakiwa na kauli mbiu ya “Mazingira Salama na Afya ni Kanuni na Haki ya Msingi mahala pa kazi”.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Afya Mahala Pa Kazi Tigo Bwn. Dismas Anthony amesema kuwa kampuni ya mawasiliano ya Tigo itaendelea kuhakikisha wafanyakazi wake wanakua na usalama na Afya mahala pa kazi ili kutoa huduma bora za Mawasiliano kwa Watanzania.

“Tigo tumejidhatiti katika hili na ndio maana mwanzoni mwa mwaka huu 2023 wafanyakazi wetu zaidi ya 400 walipewa mafunzo ya usalama na afya mahala pa kazi ili kujiimarisha zaidi katika kulinda usalama wao wakiwa kazini”.Alimalizia Bw. Dismas.

Ikumbukwe pia katika maonesho haya Tigo wameshinda pia Tuzo bora ya mpango kazi katika sekta ya Mawasiliano.

Leave A Reply