The House of Favourite Newspapers

Tigo Yamwaga Zawadi za Funga Mwaka kwa Washindi wa Kampeni ya Ndinga la Kishua

0
Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa Mary Rutta (kushoto) akimuonesha mshindi wa Vifaa vya Hisense, Dativa Thomas zawadi zake alizojishindia.

Dar es Salaam 29 Desemba 2022: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo kupitia Kampeni yake ya Ndinga la Kishua, Mamilioni ya Pesa na Vifaa vya Hisense leo imeendelea kugawa zawadi kwa washindi wa droo ya tano ya kampeni hiyo ambapo imekuwa kama zawadi ya funga mwaka kwa washindi hao.

Washindi hao waliondoka pesa taslimu shilingi milioni tano, shilingi milioni moja moja na seti ya vifaa vya Hisense ambayo ni friji, Tv ya kisasa inchi hamsini, spika za muziki wa kisasa (sound bar)na microwave.

Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Ruta (kushoto) akimpongeza mshindi wa shilingi milioni tano, Benson Reuben wakati akamkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano alizojishindia. Anayeshuhudia (katikati) ni Afisa wa Kampuni Hisense, Joseph Mavula.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta amesema kampuni hiyo inafuraha kuwapata washindi hao ambao wamepatikana kwa kufanya miamala ya Tigo Pesa na kuwataka watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo na kufanya miamala ya Tigo Pesa ili na wao waingie kwenye droo inayoendelea ambapo mwisho wa droo mshindi ataibuka na Ndinga la Kishua aina ya Toyota Rush mpya kabisa.

Mary aliendelea kusema;

Mshindi wa milioni tano, Benson Reuben (wapili kulia) akiwa na washindi wa shilingi milioni mojamoja baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi wa pesa walizojishindia walipokuwa wakikabidhiwa pesa zao.

“Leo tuko katika hafla nyingine ya kutoa zawadi kwa washindi wetu wa kampeni yetu Ndinga la Kishua, tumeshafanya droo tano na ya funga mwaka kutafuta washindi wanne wa milioni tano kila mmoja na mpaka sasa tumeshatoa jumla ya milioni 60, kwenda kwa washindi wetu na bado kuna pesa zingine shilingi milioni 54 tutazitoa kwa katika wiki tatu zijazo.

“Kwahiyo tunaendelea kuwasihi wateja wetu endeleeni kufanya miamala ya Tigo Pesa ili kuweza kujishindia milioni moja moja za kila wiki pamoja za zile zawadi kubwa za shilingi milioni kumi na milioni 20 pia utaweza kujishindia seti ya Vifaa vya Hisense kila wiki ambavyo ni Tv ya kisasa yenye nchini 50, friji, spika za muziki za kisasa (sound bar) na microwave.

“Pamoja na zawadi zote hizo pia kuna zawadi kubwa kabisa ya Ndinga la Kishua aina ya Toyota Rush mpya kabisa ambayo haijawahi kutumika ‘ziro kilomita’ ili kuweza kujishindia zawadi hizo fanya miamala mingi uwezavyo kama vile kulipa bili, kutuma na kupokea pesa, kupokea na kutuma pesa kutoka benki au mitandao mingine au nchi za nje pamoja na kufanya malipo ya serikali chukua mikopo kutoka huduma yetu ya Nivushe na Bustisha ili ujiongezee nafasi ya kuwa mshindi”. Alimaliza kusema Mary.

Kwa upande wake Afisa wa Hisense, Joseph Mavula akikabidhi vifaa Hisense kwa mshindi alisema;

“Siku ya leo kampuni yetu inayofuraha kutoa vifaa vya Hisense kwa washindi wa kampeni hii ya Ndinga la Kishua, Mamilioni ya Pesa na Vifaa vya Hisense kwani mpaka leo tuna washindi wa droo ya tano lakini nafasi bado ipo hivyo nawasihi watumiaji wote wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo na kufanya miamala ya Tigo Pesa ili kuweza kuibuka na zawadi hizi ambapo mpaka sasa bado tuna nafasi tatu kwa washindi wa vifaa vya Hisense.

“Pia nawakumbusha wananchi wote kwa ujumla kuwa maduka yetu yote ya Hisense yaliyoidhinishwa yanaendelea kutoa ofa ya asilimia 20 kwa vifaa vyetu ambapo mteja atatakiwa kukunua kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Simu”. Alisema Mavula na kumalizia kwa kuwatakia Wananchi wote heri ya sikuu ya krismas na mwaka mpya.

Kwa upande wa washindi hao, Benson Reuben ambaye ni mmoja kati ya washindi wa shingi milioni tano amesema anaishukuru sana kampuni ya Tigo kupitia kampeni yake hiyo ya Ndinga la Kishua, Mamilioni na fedha na vifaa vya Hisense kwani hakutegemea kama bahati hiyo ingemuangukia haswa katika kipindi hiki cha kufunga mwaka na kuuanza mwaka mpya ambapo yanahitaji mahitaji mengi sana ikiwemo ada na sare za wanafunzi na majukumu mengine.

Mshindi wa Vifaa vya Hisense, Dativa Thomas yeye amesema anaishukuru sana Tigo kwa kumfanikisha kushinda vifaa hivyo jambo ambalo hakulitegemea hivyo aliwasihi wateja wengine nao kufanya miamala ya Tigo Pesa kadiri wawezavyo ili nao kuweza kujishindia kama yeye na pengine zawadi kubwa ya Ndinga la Kishua Toyota Rush au mamilioni ya pesa.

Leave A Reply