TIGO YANG’ARISHA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SADC
NCHI za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), zipo katika mkakati wa kuwa na mfumo satelaiti ambao utawezesha taarifa za nchi hizo kudhibitiwa katika ukanda huo bila kuvuka mipaka.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana jijini Dar es Salaam.
Kamwelwe ameema kwa muda mrefu nchi za SADC zimekuwa zikitumia mfumo wa satelaiti ambao unahitaji taarifa kwenda katika nchi za Ulaya na Marekani ndipo zirudi nchini na kumfikia mhusika, hivyo wanataka kuondokana na utaratibu huo.
Comments are closed.