The House of Favourite Newspapers

Tigo yatoa zawadi kwa Mawakala waliofanya vizuri mwishoni mwa mwaka 2018

Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). 
Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed, (kushoto) akimkabidhi Said Khatibu (kulia) ambaye ni mmoja kati wa mawakala watano wa Tigo Pesa watano walioibuka washindi wa shilingi milioni 2 kutoka kanda ya Pwani katika Promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama
…Sayed, (kushoto) akimkabidhi Hajira Saidi(kulia) ambaye ni mmoja kati wa mawakala watano wa Tigo Pesa  walioibuka washindi wa shilingi milioni 2 kutoka kanda ya Pwani. 
Hussein Sayed, akifurahia jambo na mshindi wa jumla wa Promosheni ya Chifu wa Mawakala, Vicky Ibrahim wakati akimkabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 20. 
Washindi wa Promosheni ya Chifu wa Mawakala kutoka kanda ya Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa huduma ya Tigo Pesa kutoka kampuni ya Tigo.

 

Kampuni ya Tigo Tanzania, imetoa zawadi ya fedha taslimu kwa mawakala wake wa Tigo Pesa
waliofanya vizuri katika promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama “Wakala
Chief Promotion”.

Kupitia promosheni hiyo, wakala aliyefanya vizuri kuliko wote nchini, amepokea zawadi ya
fedha taslimu shilingi milioni 20 wakati mawakala wengine wanaofuatia kwa kufanya vizuri
kutoka kanda nne wakipokea jumla ya shilingi milioni 40.

 

Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi zao, Mkuu wa Huduma za
Kifedha wa Tigo Hussein Sayed alisema promosheni hiyo imewekwa maalum kwa ajili ya
kuwashukuru na kuwazadia mawakala wanaofanya vizuri katika kipindi cha mwisho wa mwaka.

 

Hussein alisema, washindi 20 kutoka kanda nne ambazo ni Pwani, Kusini, Kaskazini na Kanda ya
Ziwa walipatikana ambapo kila kanda ilitoa washindi watano ambao kila mmoja alijinyakulia
zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili wakati mshindi wa jumla akiondoka na shilingi
milioni 20.

“Jumla ya mawakala 90,000 walishiriki katika promosheni hii ya nchi zima iliyoanza tarehe 1
Disemba na kumalizika tarehe 31 Disemba 2018,” alisema
Kwa upande wake Mkuu wa Bidhaa Huduma za Kifedha kwa njia ya Simu, James Sumari
aliongeza kwa kuwashukuru Mawakala kwa mchango wao mkubwa katika kufikisha huduma za
kifedha kwa wantanzania.

 

“Tunayofuraha kutoa mchango unaowezesha wananchi wengi kufikiwa na huduma za kifedha.
Kupitia huduma ya Tigo Pesa, tumewawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma na kupokea
fedha na kufanya malipo mbali mbali kwa urahisi na kwa usalama. Tigo Pesa ni zaidi ya
suluhisho kwa malipo na huduma rahisi za kifedha, ni sehemu ya maisha,” alisema Sumari.

 

Vicky Ibrahim ambaye ni mshindi mkubwa katika promosheni hiyo kutoka Kanda ya Pwani mkoa
wa Dar es Salaam alisema, shilingi milioni 20 alizojishindia zitamsaidia kupanua biashara yake
hiyo ya Tigo Pesa huku akiishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo.
“Ninayo furaha kubwa kupokea zawadi hii ambayo kimsingi sikuitarajia. Nitatumia fedha hizi
kupanua biashara yangu na kutatua matatizo yangu binafsi ambayo yanahitaji fedha,” alisema

Comments are closed.