The House of Favourite Newspapers

Tigo Yawakabidhi Mkwanja Mawakala Waliojishindia Promosheni ya Malengo

0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza kwenye hafla ya kuwakabidhi zawadi zao mawakala waliojishindia kwenye promosheni hiyo.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                              

KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo, leo Jumanne Julai 12 mwaka 2022 imewazawadia mawakala wake pesa taslimu waliojishindia kwenye promosheni maalum ya malengo iliyoanza mwezi wa sita.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili wakala, Zaidi Muhidini Michuzi wa Fedha Investment baada ya kuibukia mshindi wa kwanza Kanda ya Pwani.

 

 

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari wakati wa kuwakabidhi washindi hao zawadi zao Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema;

Wakala aliyeibuka mshindi wa pili Kanda ya Pwani, Ferdinand Joseph kutoka duka liitwalo Paulo Msaki naye akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni moja aliyojishindia.

 

 

“Napenda kuwakaribisha wageni waalikwa kwenye kwenye hafla hii ya kuwazawadia mawakala wetu ambao wameendelea kufanyakazi na sisi katika promosheni hii maalum iliyoanza tangu mwezi wa sita ambayo iliwapa mawakala wetu chachu ya kufanya miamala zaidi.

 

“Leo hii tunayofuraha kuwazawadia mawakala tofauti walioweza kuibuka washindi, hii ilikuwa ni promosheni ya kimkakati iliyokuwa na lengo la kuongeza chachu kwa mawakala wetu nchi nzima”. Amesema Angelica. Akiendelea kufafanua zaidi Angelica amesema;

 

Mshindi wa Kwanza Kanda ya Pwani, Zaidi Michuzi (wa pili kushoto) akiwa na maofisa wa Kampuni ya Tigo wakati akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili alizojishindia.

 

 

“Kati ya mawakala wetu zaidi ya laki na hamsini nchi nzima tumekuwa na washindi zaidi ya elfu moja ambao walikuwa wakishindania milioni 140. Promosheni hii ilikuwa ikimpa wakala lengo kufikia kutokana na miamala anayofanya kila siku”.

 

“Kwa hiyo mawakala wetu tumewapa malengo tofauti na hivyo wale walioshinda katika malengo hayo ndiyo leo hii tunawapa zawadi zao na hapa tupo na wawakilishi kadhaa. “Promosheni hii tumeigawanya katika kanda tano ambapo kuna kanda ya Pwani, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Zanzibar, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kusini.

 

“Hivyo katika washindi hao, 1000 pia tuna washindi wakuu wawili katika kila kanda ambapo mshindi wa kwanza anajipatia zawadi ya shilingi milioni mbili na mshindi wa pili anazawadiwa shilingi milioni moja. Hivyo tunawaomba mawakala wetu pamoja na wateja wetu wanaotumia huduma ya Tigo Pesa kufanya miamala na malipo mbalimbali ikiwemo huduma za kiserikali waendelee kufanya kazi nasi.

 

Tigo Pesa ni zaidi ya pesa.” Alimaliza kusema Angelica. Akizungumza baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili alizojishindia Wakala wa Tigo Pesa,  Kutoka Kampuni ya Fedha Investment, Zaidi Muhidini Michuzi amesema anaishukuru sana kampuni ya Tigo kupitia huduma yao ya Tigo Pesa ambapo katika promosheni hiyo iliyowapa malengo ya kufikia na walivyoyafikia ofisi yake imejishindia kitita cha shilingi milioni mbili.

 

“Napenda nitoe shukrani nyingi sana kwa kampuni ya Tigo kwani kiasi hiki kitasaidia kuongeza mtaji wa biashara yangu”. Alisema wakala Zaidi Muhidini Michuzi aliyeibuka mshindi wa kwanza kwa kanda ya Pwani inayohusisha mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

 

Naye mshindi wa pili kanda ya Pwani, Wakala Ferdinand Joseph ambaye ofisi yake inatambulika kwa jina la uwakala la Paulo Msaki  ambaye amejishindia shilingi milioni moja amesema anaishuru sana kampuni ya Tigo kwa promosheni hiyo na kuwashauri mawakala wenzake na kushiriki kiufasaha promosheni hiyo ili nao waweze kujishindia kama wao.         

Leave A Reply