The House of Favourite Newspapers

Etihad Yazindua Mfumo wa Kisasa wa Usimamizi wa Mizigo Viwanja vya Ndege

0

Etihad Airways' Boeing 787 set to fly to five further destinations in 2016

Shirika la ndege la Etihad ambalo ndio shirika rasmi la nchi ya Falme za kiarabu, leo hii limetangaza makubaliano na kampuni ya Luggage Logistics kuboresha mfumo mzima wa usimamizi wa mizigo katika viwanja vake vya ndege dunia nzima.

Kupitia mfumo wa kisasa wa Baggage Management System (BMS) unaosimamiwa na kampuni ya Luggage Logistics, shirika la ndege la Etihad litaweza kuboresha usimamizi ikiwemo kusafirisha mizigo ya wasafiri kwa wakati. Mfumo huo pia utawezesha kufuatilia kwa urahisi mizigo iliypotea njiani dunia nzima.

Mfumo wa BMS utahusisha ratiba za ndege, taarifa za wasafiri pamoja na mifumo ya udihibiti safari zote ka pamoja. Hii itasaidia kuongeza kasi taratibu za kutambua mizigo ya abiria  na kisha kuhamisha mizigo toka kwenye ndege hadi uwanja wa ndege na hatimaye kwenda kwenye ndege ya kuunganisha safari husika, ikisaidia safari kutochelewa.

Mfumo huu umeunganishwa katika kituo kimoja cha udhibiti ambapo taarifa zote za mizigo kutoka vyanzo mbalimbali hutunzwa. Taarifa hizi zinaweza kusambazwa haraka na uwepesi baina ya vitengo husika dunia nzima

Geert W. Boven, Makamu rais wa Huduma za viwanja vya ndege kutoka Etihad, alisema: “Ushirikiano na kampuni ya Luggage Logistics kutaongeza ufanisi zaidi katika kutambua, kusimamia na kusafirisha mizigo ya abiria duniani kote kwenye viwanja vyetu tukianzia na hapa Abu Dhabi. Mfumo mpya huu utasaidia kuboresha huduma kwa abiria kwa kupunguza upotevu wa mizigo, kupunguza idadi ya safari zinazochelewa juu ya kupotea kwa mizigo pamoja na kuongeza ufanisi wa huduma zetu za uwanja wa ndege”

Adam Dalby, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Luggage Logistics, alisema “Tunayofuraha kushirikiana na shirika la ndege la Etihad, shirika ambalo tupo pamoja katika kutambua umuhimu wa uvumbuzi na huduma bora. Kupitia mfumo huu wa kisasa wa BMS, taarifa za papo hapo hupatikana na hutumika kuhakikisha mizigo ya abiria inasimamiwa kwa ufanisi zaidi safari nzima”

Shirika la ndege la Etihad lilichagua mfumo wa BMS kwani unakidhi mahitaji na vigezo vyote vya usimamizi mizigo, ikiwemo ICAO Annex 17 pamoja na maazimio ya IATA, mfumo huu unaweza kuunganishwa na mitambo ya shirika hili la ndege bila ugumu wowote pia. Suluhisho hili limewiana na uendeshaji na mahitaji ya miundombinu ya Shirika la ndege nay ale ya kituo cha Abu Dhabi

Leave A Reply