TIKO: 2019 NATAKA MUME, NIMECHOKA KUSUBIRI

 

Tiko Hassan

MWANAMUZIKI ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan amesema yeye kama mwanamke aliyeka­milika mwaka huu wa 2019 anaomba sana ili apate mume maana amechoka kusubiri. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Tiko alisema kuwa ndoa ni heshima kwa kila mwanamke na amesubiri kwa muda mrefu bila mafanikio lakini imani yake ni kwamba, atauona mwaka wa 2020 akiwa ni mke wa mtu.

“Jamani nimechoka kusubiri lakini naamini mwaka huu utakuwa ni mzuri kwangu, kila kwenye ibada namuomba Mungu anijaalie mume bora ndani ya mwaka huu,” alisema Tiko.

STORI: Mwandishi Wetu, Ijumaa WikiendaTecno


Toa comment