The House of Favourite Newspapers

TIKO AWATAKA MASTAA KUHESHIMU SERIKALI

MREMBO wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Tiko Hassan ameibuka na kuwataka mastaa wenzake kutii serikali pindi wanapoitwa kwa ajili ya kazi zao za sanaa na siyo kudharau.

Akistorisha na Za Motomoto News, Tiko alisema kuwa, serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imekuwa ikiwaita baadhi ya mastaa hasa wa muziki na wale wanaokaa nusu utupu mitandaoni kwa ajili ya kuzungumza au kurekebisha kazi zao, lakini wengi wao wanadharau, jambo ambalo siyo sawa.

“Jamani mastaa tunatakiwa tuheshimu serikali, tusidharau pale tunapoitwa bali tunatakiwa kutii wito kwani itatusaidia sana katika kazi zetu,” alisema Tiko.

Comments are closed.