The House of Favourite Newspapers

Tiko: kujuana kunaua filamu

tikoooooooooMsanii wa filamu Bongo, Tiko Hassan.

Na gladness mallya

MSANII wa filamu Bongo, Tiko Hassan ameibuka na kulilia tabia za mastaa wa fani hiyo kuleta kujuana kwenye kazi kitu kinachochangia kwa kiasi kikubwa kuua sanaa hiyo kwa vile wenye vipaji wanaachwa.

Akipiga stori na Risasi Mcha nganyiko, Tiko alisema watu wanapokuwa na kazi zao, huwachukua wasanii wanaowafahamu hata kama hawajui kucheza na kuwaacha wazoefu wenye vipaji, kitu ambacho kinadidimiza sanaa na kuonekana hazina kitu kipya.

“Jamani ndiyo maana wasanii wengi wamekuwa hawasikiki tena kutokana na kwamba hawana uwezo wa kutengeneza kazi zao wenyewe, wanategemea kushirikishwa lakini ndiyo hivyo wanawachukua wale wanaowafahamu au hata ndugu zao,” alisema Tiko.

Comments are closed.