The House of Favourite Newspapers
gunners X

Timbwili Kortini: Mmiliki wa Shule ya Scolastica na Baba wa Marehemu – Video

SHUGHULI ilikuwa pevu wakati mmiliki wa Shule ya Scolastica, Edward Shayo akipelekwa gerezani jana, ilikuwa ni tafrani kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Moshi na kusababisha polisi kutumia nguvu kumdhibiti baba mzazi wa mtoto aliyeuawa.

 

Jackson Makundi ambaye ni baba wa Humphrey Makundi aliyeuawa usiku wa Novemba 6,2017 na maiti yake kutupwa mto Ghona, alifika mahakamani hapo saa 9:40 alasiri na kukosa nafasi ya kuingia ndani ya mahakama.

 

Ndani na nje ya chumba cha mahakama kulikuwa na idadi kubwa ya watu kiasi kwamba, baadhi ya wasikilizaji walilazimika kusimama ndani na nje ya mahakama.

Baada ya Mahakama kumalizika na washitakiwa wakiwa wanapelekwa katika gari la polisi ili kupelekwa Gereza la Karanga, ndipo Shayo alipowapungia mamia ya watu huku akiwaaga.

 

Ni katika kipindi hicho alimuona baba wa marehemu na kutamka maneno kuwa, “Makundi damu ya mtoto wako hainihusu”, maneno yaliyoibua hasira kwa mzazi na kutaka kwenda kumshambulia.

 

“Unasemaje?” alisikika Makundi akiuliza huku akielekea kwenye gari ya polisi hali iliyoibua kelele za kurushiana maneno kati ya ndugu, jamaa na marafiki wa makundi na wale wa upande wa Shayo.

 

Mahakama Kuu Kanda ya Moshi ilimuhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa mlinzi wa Shule ya Sekondari Scolastica, Hamis Chacha, baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi Humphrey Makundi huku mmiliki wa shule hiyo, Edward Shayo na aliyekuwa mwalimu wa nidhamu, Labani Nabiswa wakihukumiwa kifungo cha miaka minne jela kila mmoja wa kosa la kuficha ukweli wa mauaji hayo.

TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.