The House of Favourite Newspapers

Timu Diamond, It’s Too Much Sasa, Muacheni Hamisa!

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’

UHUSIANO wa ki­mapenzi kati ya msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwanadada Hamisa Mobeto ndiyo ishu inayozidi ‘ku-make headlines’ kila kukicha.

Baada ya Diamond kuachana na Zarina Hassan ‘Zari’, Hamisa ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya mwanamama huyo mwenye asili ya nchini Uganda lakini mapenzi yake na Diamond yame­kuwa kama mzigo wa miiba kwenye kichwa cha mwanadada huyu, anadhalilishwa sana mpaka anatia huruma. Kwa wafuatiliaji wa mambo, wanaelewa kwamba uhusiano wa Hamisa na Diamond haujaanza jana wala leo, Hamisa amewahi kukiri kwamba alikuwa kwenye uhusiano wa siri na Diamond kwa miaka zaidi ya tisa huko nyuma.

Lakini ishu ilikuja kubumbu­ruka baada ya mwanadada huyo kubeba ujauzito na baadaye kujifungua mtoto wa kiume, Dylan katika kipindi ambacho Diamond alikuwa akiendelea na mapenzi motomoto na mzazi mwenzake, Zari.

Yaliyotokea baada ya hapo wengi watakuwa wanafahamu na kwa faida ya wasioelewa, ni kwamba kitendo cha Diamond kuzaa na Hamisa wakati akiwa na Zari, kilitafsiriwa na mwanamama huyo kama usaliti mkubwa na hiyo ikawa miongoni mwa sababu za ku­sababisha ‘jini mkata kamba’ kulipitia penzi la Zari na Diamond mpaka leo zimebaki stori tu.

Diamond akawa ni kama ‘amem­kunjia’ Hamisa kwa kitendo chake cha kutoa siri kwamba mtoto ni wa Diamond na kumvurugia penzi lake na Zari, wakasumbuana sana mpaka kufikia hatua ya kupelekana mahaka­mani baada ya Diamond kugoma kutoa matunzo ya mtoto.

Baadaye suala hilo lilisuluhishwa mahakamani lakini huo haukuwa mwisho. Hasira za Diamond kumkosa Zari walizokuwa nazo watu wanaojiita Timu Diamond mitandaoni, wakazihamishia kwa kuanza kumtolea maneno yasiyofaa Hamisa na uzao wake.Wale wanaojiita Timu Zari nao wakakasirishwa kwa nini Hamisa aingilie uhusiano wa Diamond na Zari mpaka wakatengana? Nao wakawa wanamsakama mwanadada huyo kila kukicha mitandaoni.

 

Kundi jingine linalojiita Timu Wema, ambalo lilikuwa na mategemeo makubwa kwamba baada ya Zari kubwaga man­yanga, Wema Sepetu ‘Madam’ atarithi mikoba, nalo likawa na hasira na Mobeto kwa kutibua mi­pango na kuonesha kuwa beneti na Diamond.

Yote tisa, kumi ni familia ya Diamond, akiwemo mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ na dada wa Diamond, Esma Platnumz. Kwa nyakati tofauti, tena mara kwa mara, wamekuwa wakip­inga vikali uhusiano wa wawili hao huku wakitoa maneno mengi yasiyo­faa kwa Hamisa.

Ishu mpya ni baada ya juzikati mama wa Hamisa, Shufaa Rutig­inga kuhojiwa na kituo kimoja cha runinga am­bapo amefunguka kwamba Diamond amemnunulia mwanaye nyumba ya ghorofa ambayo ndipo Hamisa, Dylan na mama yake Hamisa wanapoishi hivi sasa.

Matusi anayotukanwa mwan­amke huyu, wengi wakimtuhumu kama amedanganya na matusi anayopewa Hamisa, inafika ma­hali yanakuwa ‘too much’. Una­jiuliza kwa nini watu wanaingilia sana uhusiano huu? Kwa nini Hamisa anaonekana kama adui wa kila anayempenda Diamond? Hamisa akimbilie wapi sasa?

Hamisa ni binadamu kama walivyo binadamu wengine, naye ana moyo na haya ya­nayoendelea yanamuumiza. Hivi watu wanasubiri mpaka ajikute ametopea kwenye dimbwi la matumizi ya madawa yakulevya kwa sababu ya stress ndiyo wamuonee huruma?

Wanasubiri siku wasikie ameamua kuchukua uamuzi wa kuyakatishamaisha yake (hatuombei) kwa sababu ya ku­sakamwa ndipo watu wajifanye walikuwa wanampenda? Ifike mahali huu unafiki wa mitandao­ni ufike mwisho. Hakuna aliyeku­wepo wakati Diamond anaku­tana na Hamisa, hebu waachwe kama ni kuachana waachane wenyewe kwa matatizo yao, siyo kwa sababu ya shinikizo la ndugu au mashabiki.

HASH POWER, 

MOBETO: NYUMBA TUNAYOISHI IMETOKA KWA DIAMOND – VIDEO

Comments are closed.