Kombe la FA: Chelsea Yaitandika Man United, Kukutana Na Spurs Nusu Finali
Wachezaji wa Chelsea wakiompongeza N’Golo Kante baada ya kufunga bao
Paul Pogba kwenye harakati zake akiwa uwanjani
Ander Herrera akioneshwa kadi nyekundu ya kutolewa nje ya uwanja na mwamuzi
Paul Pogba akijaribu kuwatoka wachezaji wa Chelsea
Timu ya Chelsea imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainal kwenye kombe la FA baada ya kuifunga Manchester United kwa bao 1-0 lililofungwa na N’Golo Kante dakika ya 51 jana usiku huku mchezaji wa Manchester United, Ander Herrera, akitolewa kwa kadi nyekundu.
Kutokana na matokeo hayo Chelsea itakutana na Tottenham kwenye nusu fainali, huku Arsenal itakutana na Manchester City.
Mechi zote mbili za nusu fainali zitachezwa kwenye uwanja wa Wembley wikendi ya tarehe 22 na 23.
Spurs walifika nusu fainali kwa kuilaza Millwall 6-0 Jumapili.
Arsenal, ambao walishinda kombe hilo mwaka 2014 na 2015 waliwafunga Lincoln City 5-0 Jumamosi.
Manchester City ambao wanacheza nusu fainali kwa mara ya kwanza katika misimu minne, walifuzu kwa kuilaza Middlesbrough 2-0 ugenini.
Comments are closed.