Kartra

Tishu Aliyofutia Machozi Messi Yauzwa Bilioni 2.3

AGOSTI 8, 2021 mchezaji maarufu wa soka Duniani, Leonel Messi aliwaaga rasmi viongozi, wachezaji wenzake na mashabiki wa Klabu yake ya Barcelona hiyo aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka 20 tangu akiwa kinda.

 

Wakati akiaga kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari, Messi alionekana akibubujikwa machozi, mkewe Antonella alimpa tishu na kujifuta machozi.

 

Sasa wakati ile Press Conference ilipoisha, kuna mwandishi wa habari shabiki kindakindaki wa Messi, akachukua ile tishu na kusepa nayo.

 

Jamaa kwa sasa ameiweka kwenye mtandao wa kijamii na anaiuza kwa Dola Milioni $1 sawa na Tsh. Bilioni 2.3 akiamini kuwa tishue ile ina genetic material ya Messi (maumbile) ya Messi ambayo mtu akiitumia tishu ile anaweza kuwa na nyota ya uchezaji na mafanikio katika soka kama alivyo Messi.

Kwenye mauzo hayo, ameweka pia na jezi ya Messi na watu wanaonekana kutamani kununua tishu hiyo. Taarifa hizo zimesambaa katika mitandao ya kijamii duniani kote huku watu wakihoji ni namna gani anaweza kuwahakikishia kuwa atakayetumia tishu hiyo anaweza kuwa kama Messi.

 

Kwa sasa nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Argentina amejiunga na Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka miwili.

 

Kwa takribani wiki mbili sasa tangu asajiliwe PSG, Messi ameuza mamilioni ya jezi ambapo kila jezi yake inauzwa kwa paundi 115 (Tsh 363,251) mpaka €paundi 165 (Tsh 521,187), na mpaka sasa ameshaingiza dola za Marekani milioni  100 (Tsh Bilioni 231.9) kutokana na mauzo ya jezi zake.

Messi ameshinda mataji 35 Barcelona alikodumu kwa miaka 21 tangu awasili akiwa na umri wa miaka 15 na akacheza mechi yake ya kwanza timu ya wakubwa mwaka 2004 alipofikisha miaka 16.

 

Kwa ujumla amecheza mechi 778 na kuweka rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kwa mabao yake 672, yakiwemo 120 ya kwenye Ligi ya Mabingwa na 474 ya rekodi kwenye LaLiga. Pia ameshinda mataji 10 ya LaLiga, manne ya Ligi ya Mabingwa na saba ya Kombe la Mfalme.

 

Imeandaliwa na Edwin Lindege @eddynevo


Toa comment