TMRC Yasaini Hati ya Makubaliano Kusaidia Kaya Masikini, Ridhiwani Kikwete Atoa Tamko

TAASISI ya mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortgage Refinance (TMRC) imesaini hati ya makubaliano kusaidia kaya maskini na Shirika la Kimataifa la kusaidia kaya maskini Habitat for Humanity International ikiwa ni hatua ya kwanza ya juhudi za pamoja za mashirika hayo kupanua na kuimarisha sekta ya fedha na makazi kwa watu wenye kipato cha chini nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akizungumza wakati wa utiaji wa saini alisema ushirikiano huo mpya ni hatua muhimu ya kutimiza lengo la serikali la kusaidia kaya zenye kipato duni nchini Tanzania, utafungua milango ya kifedha na kuboresha makazi kwa kaya maskini, ““Tanzania ni moja kati ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani, hata hivyo familia nyingi bado zinashindwa kupata makazi yaliyo bora”

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC Oscar Mgaya amesema:
“TMRC inaamini kuna uwezekano mkubwa mikopo ya nyumba kufikia familia maskini, Sisi kama wakopeshaji tuna hamu yakujenga nyumba za gharama ndogo ili hata wenye kipato duni waweze kufaidika na mikopo hii”, chini ya ushirikiano huo mpya Habitat for Humanity International itatoa msaada wa kiufundi kwa TMRC ili kuwezesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ili kila Mtanzania aweze kufaidika.

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.