The House of Favourite Newspapers

TMZ Yazindua ‘Documentary’ ya Maisha ya Sean ‘Diddy’ Combs

0
Sean ‘Diddy’ Combs

Mtandao maarufu wa burudani duniani, TMZ umezindua ‘documentary’ ndefu ya maisha ya Sean ‘Diddy’ Combs iliyopewa jina la Downfall of Diddy: The Indictment ambayo inaelezea kwa kina maisha ya staa huyo mpaka alipokamatwa na polisi kutokana na tuhuma kadhaa zinazomkabili.

Hapo jana, TMZ waliachia kipande kifupi cha sehemu ya documentary hiyo kwenye tovuti yao ikielezea mlolongo wa mashtaka yanayomkabili Diddy anayeshikiliwa kwenye Gereza la Metropolitan, Brooklyn jijini New York kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono pamoja na usafirishaji wa binadamu.

TMZ imeeleza kuwa imechimbua kwa undani simulizi ya kila kilichotokea kutoka kwa watu wa karibu wa Diddy waliokuwepo kwenye matukio mbalimbali yaliyomsababishia matatizo ambapo documentary hiyo inatajwa kuwa itafichua mambo mengi yasiyokulikana na yaliyojificha aliyokuwa akiyafanya mshindi huyo wa Tuzo tatu za Grammy.

Wakati hayo yakiendelea baadhi ya picha zimesambaa mitandaoni, zikimuonyesha mzazi mwenza wa P Diddy, Dana Tran, akiwa na mtoto wake Love Sean Combs, huku akiwa amevalia Pete ya ndoa jambo lililotafsiriwa kama Kumuunga mkono Diddy na Kuonyesha heshima kwake.

KESI ya BONI YAI NGOMA NGUMU – ASOTA TENA GEREZANI BAADA ya DHAMANA KUGONGA MWAMBA…

Leave A Reply