Tofauti Ya Eid Ul-Fitr Na Eid Ul-Adha

LEO (Julai 21) Waislamu kote nchini wameungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Eid ul-Adha ambayo kwa wengine huiita Idd Kubwa.

 

Pamoja na kuwatakia heri Waislamu katika siku yao hii njema, jambo ambalo pengine wasiofahamu wangependa kujua; tofauti ya Sikukuu ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha ni ipi?

 

EID UL-FITR

Ingawa ni kwa ifupi, Eid ul-Fitr maana yake ni “Sikukuu ya Kumaliza Mfungo” na huadhimishwa mwisho wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

 

Kabla ya ibada hiyo, Waislamu huwa wanatoa sadaka kwa maskini na sadaka hiyo ‘huitwa Zakat’ ambayo ni moja ya nguzo kuu katika dini ya Kiislamu.

Siku hii huadhimishwa baada ya kuonekana kwa mwezi wa Shawwal na kufuatiwa na sherehe zinazoambatana na mapumziko ya kitaifa kwenye nchi nyingi.

 

EID UL-ADHA

Eid al-Adha maana yake ni “Sikukuu ya Kutoa Kafara/Kuchinja” Hutumiwa kukumbuka wakati Nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ishmael kama alivyoamriwa na Allah, alipotii Mungu alimpatia kondoo amtoe kafara badala ya mwanaye.

 

Sikukuu ya Eid ul-Adha huadhimishwa kuanzia siku ya 10 tangu kuonekana kwa mwezi wa Dhul Hijjah.

Waislam huisherehekea kwa kuchinja wanyama na kutoa sadaka kwa wahitaji huku msingi wake mkuu ukiwa ni kuonesha utiifu mbele ya Mwenyezi Mungu ambao Nabii Ibrahimu alianza kuuonesha.


Toa comment