The House of Favourite Newspapers

TOP 5 MASTAA WAKIKE WANAOKIMBIZA BONGO FLEVANI

Lulu Abbas ‘Lulu Diva’

BONGO kwa sasa kuna wanamuziki wa kike wengi ambao kazi zao zinafika mbali na wanafanya vizuri, hii chini ni Top 5 ya Ijumaa, ambapo imezingatia ukubwa wa kazi zao na namna zinapenya kwa mashabiki.

  1. LULU DIVA

Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anaingia kwenye Top 5 akikaa namba tano hasa kutokana na ngoma yake ya Ona aliyomshirikisha Rich Mavoko kufanya vizuri zaidi. Wakati Lulu anatoka kimuziki na Ngoma kama Homa, alikuwa na ushindani mkubwa na wanamuziki ambao alianza nao kwenye mambo ya kuuza sura kwenye video, akiwemo Amber Lulu na Gigy Money. Lakini mapokeo ya kazi yake hii yamefanya apige hatua moja mbele ya wanamuziki hao.

  1. RUBY

Ni mwanamuziki mkali na anajua. Miaka michache iliyopita tungeweza kumpa hata namba moja kwenye listi hii kutokana na uwezo wake. Lakini baada ya hapa katikati kupotea kabla hajarudi na kuibuka na Wimbo wa Ntade, kuna wanamuziki walimpita na kuchukua namba yake. Kwenye listi hii anachukua namba ‘foo’.

  1. MAUA SAMA

Mwaka 2015, Maua Sama alipotoa Wimbo wa So Crazy akimshirikisha MwanaFA, ndipo mashabiki wengi walimuelewa mwanadada huyu. Nakumbuka kuna baadhi ya mashabiki mitandaoni walisema ndiye ‘Besta’ wa Kizazi Kipya.

Nyimbo zake za Sisikii na Mahaba Niue zilizidi kupigilia msumari kwenye mbao zinazoshikilia safina ya muziki wake na sasa anatamba na Wimbo wa Amen akiwa amem-

shirikisha Ben Pol. Ijumaa inampa namba tatu, kwa sababu pia ni mwanamuziki mzuri mwenye uwezo wa kuwasapoti wanamuziki wenzake wanapom- shirikisha kwenye kolabo. Unaweza ukacheki nyimbo kama Love Me ya Stamina na nyingine alizoshirikishwa.

  1. NANDY

Baada ya kuibuka na kufanye Wimbo wa Gusa Gusa na One Day kisha Kivuruge, wengi walianza kumfa- nanisha na kumshi- ndanisha mwanadada Faustina Charles ‘Nandy’ na Ruby. Kwamba anafanana naye kwenye uimbaji na midondoko kwenye biti.

Labda pengine kwa sababu wote ni zao la Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT). Hata hivyo baadaye taratibu Nandy alianza kupenya, baada ya Ruby kupotea kwa muda akachukua gemu lake. Nyimbo zake za Ninogeshe, ‘cover’ ya Nikumbushe, Wimbo wa Njiwa alioshirikiana na Willy Paul na nyimbo alizoshirikiana na Aslay kama vile Subakheri Mpenzi zimemuweka mahala pazuri kwenye gemu na Ijumaa linampa namba mbili.

  1. VEE MONEY

Vanessa Mdee ‘Vee Money’ huyu ni mama yao kwa sasa. Ndiye namba moja kwenye listi hii. Amefanya kazi nyingi ambazo si tu kawafunika wanamuziki wa kike Bongo, bali hata wanamuziki wa kiume. Kafanya ngoma na KO ambaye ni mwanamuziki mkubwa tu Afrika iitwayo No Body But Me, kafanya kazi na Cassper Nyovest, amefanya kazi na Navio, kafanya kazi na Diamond Platnumz na anamiliki albamu iitwayo Money Mondays, ambayo imefika mbali pia.

Lakini kama haitoshi, Vee Money amebahatika kupata tuzo 11 ambapo kati yake kuna tuzo kubwa kama MTV Music Awards, MTV VJ na kashindanishwa kwenye tuzo nyingi na kuiletea heshima Bongo Fleva kwa upande wa wanawake nje ya nchi.

Lulu Diva

MAKALA: BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.