The House of Favourite Newspapers

TOP FOUR; HAINA MWENYEWE KWENYE PREMIER LEAGUE MSIMU HUU

KWA hali ilivyo kwa sasa ni wazi kwamba hakuna aliyejihakikishia kumaliza nafasi nne za juu kwenye Premier League msimu huu.

 

Premier ndiyo ligi pendwa duniani na imekuwa ikifuatiliwa na mabilioni ya mashabiki kila wikiendi hii yote ni kutokana na ugumu wa ligi yenyewe.

 

Vita kubwa huwa inakuwepo kwenye zile timu zinawazowania kumaliza katika nafasi nne za juu lengo lao likiwa ni kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’ msimu unaofuatia.

 

Hiko kimekuwa kikichochea kwa nguvu zaidi ushindani. Angalia wakati fulani msimu huu Liverpool imewahi kuongoza kwa zaidi ya pointi saba zaidi ya timu inayomfuatia lakini sasa Man City imewakuta.

Wikiendi hii tena kutakuwa na mtiti wa nguvu ambapo vigogo wa timu sita za juu watakuwa wanaskaa alama muhimu za kuwaweka pazuri kwenye mbio za kwenda top four.

ARSENAL
Arsenal ambao wapo nafasi ya sita kwa sasa, leo watakuwa ugenini kucheza na watoto wa Kocha David Wagner, Huddersfield ambao wapo mkiani mwa ligi.
Arsenal licha ya msimu huu kutokuwa na rekodi nzuri ugenini, imekutana na mara tatu na Huddersfield na Gunners wameshinda michezo yote.
Arsenal ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 25 ambapo imeshinda 15, sare tano na kuchapwa sita, mefunga mabao 51 na kufungwa 36. Ikishinda mechi inayofuata itakwenda hadi nafasi ya nne.

 

MAN UNITED
Man United inayonolewa na Kocha Ole Gunnar Solskjær leo Jumamosi itakuwa ugenini kuwakabili Fulham ambao wanapambana kubaki Premier saa 9:30 Alasiri. United imetinga kibishi nafasi ya tano baada ya kufanya hivyo kwenye mechi nane mfululizo ambapo ya tisa wakatoa sare na ya 10 wakashinda.
United ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 48 ilizozipata baada ya kucheza mechi 25 ambapo imeshinda 14, sare sita na kufungwa mitano, imefunga mabao 49 na kufungwa 35, ikishinda mechi yao itakwea hadi nafasi ya nne.

CHELSEA
Watoto wa Maurizio Sarri wanaonekana kuurejesha morali baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Huddersfield wikiendi iliyopita. Kesho Jumamosi watasafiri hadi mjini Manchester kuwavaa Man City kwenye Uwanja wa Etihad.
Ni game ngumu kwa timu zote kutokana na uimara wa vikosi. Yeyote atakayepigwa maana yake anaweza kushushwa kwenye nafasi aliyopo sasa hivi kama wapinzani wao watashinda.
Chelsea wenyewe wapo nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 25, wanapointi 50 ilizozipata baada ya kushinda mechi 15, sare tano na kuchapwa mara tano huku ikifunga mabao 45 na yenyewe ikifungwa 23.

TOTTENHAM
Kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino ana kazi ngumu kesho dhidi ya Leicester City ambayo nayo inataka kumaliza nafasi 10 za juu.
Spurs ambayo ipo nafasi ya tatu baada ya kushinda mechi 19 na sare sita ikiwa na pointi 57, kama itashinda mchezo huu itafikisha alama 60 hivyo kuzidi kuzisogelea City yenye 59 na Liver wenye 62 kileleni.
Spurs licha ya kukosa huduma ya nahodha wake, Harry Kane imezidi kuthibitisha kuwa inaweza kwani mpaka sasa imefunga mabao 51 na kuruhu 24 tu na bado inatoa upinzani mkali top four.

 

MANCHESTER CITY
Man City inaonekana safu yake ya ushambuliaji ndiyo bora Premier ikiwa imefunga 68 kuliko timu zote wikiendi hii itakuwa nyumbani kuwasubiri Chelsea pale Etihad.
Ikishinda mchezo huu basi itaendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Liverpool hata kama itashinda dhidi ya Bournemouth leo.
Mpaka sasa City ina pointi 62 ilizozipata baada ya kucheza mechi 26 ambapo imeshinda 20, sare mbili na kupoteza nne huku ikifunga mabao 68 na kufungwa 20 tu.

 

LIVERPOOL
Itakuwa inajilaumu kutokana na kuruhusu ‘gape’ la zaidi ya pointi tano kukutwa. Usiku wa kumakini juzi walishushwa hadi nafasi ya pili na City na pointi zao 62.

Katika michezo 25 waliyocheza wameshinda 19, sare mitano na kupoteza mmoja tu, wamefunga mabao 56 na kufungwa 15 tu, hii ndiyo timu iliyofungwa mabao machache Premier mpaka sasa. Sasa cheki takwimu kwa timu zilizopo TOP FOUR mpaka sasa;

1111111111111111111111111111
Liverpool
#Tangu Ligi ya England ibadilishwe kutoka Ligi Daraja la Kwanza na kuwa Premier League Liver hawajawahi kutwaa ubingwa huo.

Usahihi wa pasi 85%
Usahihi wa krosi 24%
Usahihi wa mashuti 42%

#Liverpool inamtegemea zaidi Salah kwenye kutupia mabao ambapo mpaka sasa amefunga 16 na ndiyo kinara Premier

#Liver ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mechi kwenye uwanja wake wa nyumbani, katika mechi 12 imeshinda 10 na sare mbili.

Pasi 15, 742
Mashuti 372
Krosi 453

VINARA WA MABAO
Salah 16
Mane 11
Firmino 6
#KOCHA Jurgen Klopp

111111111111111111111
MANCHESTER CITY
Pasi 18,185
Mashuti 448
Krosi 525

#City imeshinda mechi 13 kati ya 14 zilizopita ilizocheza uwanja wa nyumbani.

#City inajivunia safu yake ya ushambuliaji ya SAS ambayo kwa pamoja imefunga mabao 32 katika michezo 25.

Sergio Aguero 14
Raheem Sterling 10
Leroy Sane 8

#Ina wastani wa kufunga mabao mawili katika mechi 14 zilizopita ambazo walicheza uwanja wa nyumbani.

#Inatumia uwanja wa Etihad unaobeba mashabiki 55,097

Usahihi wa pasi 89%
Usahihi wa krosi 20%
Usahihi wa mashuti 39%

#City ndiyo timu kinara wa kupiga pasi, mpaka sasa imepiga 18,185.
#KOCHA Pep Guardiola

MECHI ZAO ZINAZOFUATA
Man City v Chelsea
Man City v West Ham
Bournemouth v Man City
Man City v Watford
Man Utd v Man City
Fulham v Man City
Man City v Cardiff
Crystal Palace v Man City
Man City v Spurs
Burnley v Man City

TOTTENHAM
Pasi 14,164
Mashuti 338
Krosi 435

# Tottenham imeshinda mechi tisa kati ya 11 zilizopita kwenye Premier

#Katika mechi tatu zilizopita imeshinda kwa tofauti ya bao moja tu

Usahihi wa pasi 84%
Usahihi wa krosi 27%
Usahihi wa mashuti 39%

WANAOONGOZA KWA MABAO
Kane 14
Son Heung-Min 10
Lucas Moura 6

# Christian Eriksen ndiye kinara wa kutoa asisti kikosini humo, katoa nane

#Tottenham inatumia Uwanja wa Wembley ambao unabeba mashabiki 90,000
#KOCHA Mauricio Pochettino

11111111111111111111111
CHELSEA
# Eden Hazard wa Chelsea ndiye kinara wa asisti Premier akiwa amepiga 10 huku akifunga mabao 12.

VINARA WA PASI CHELSEA
Jorginho 2,219
Antonio Rüdiger 1,986
David Luiz 1,893

Usahihi wa pasi 88%
Usahihi wa krosi 19%
Usahihi wa mashuti 34%

#Katika timu nne za juu, Chelsea ndiyo imefunga mabao machache zaidi ambayo ni 45.

#Uwanja wa Stamford Bridge ambao unatumiwa na Chelsea unabeba mashabiki 41,631
Kocha Maurizio Sarri

Comments are closed.