TOP SKENDO SKENDO ZA MASTAA BONGO 2018

Zarina Hassan ‘Zari’

KWENYE dunia ya mastaa kuna mengi. Yapo ya kuburudisha, kuelimisha na mengine yatakuacha mdomo wazi. Kuna vitimbi na vituko! Kubwa zaidi ni skendo za kila kukicha.

 

Huko baadhi ya mastaa wamekuwa wakikumbwa na skendo. Lakini cha ajabu baadhi yao wamekuwa wakifurahia na kuona kama ni sehemu ya kuwapaisha bila kujali kuchafuka na kupoteza heshima mbele ya macho ya jamii.

Wapo wanaoamini kuwa kukumbwa na skendo ni kutengeneza ‘attention’ ili iwe rahisi kufuatiliwa kwa kazi zao za sanaa bila kujua kwamba kazi nzuri ‘inajiuza’ yenyewe na kutegemea skendo ni kujidhalilisha.

Zari na Diamond.

Kama nilivyosema, baadhi yao hawajali hata kidogo kuwa huko ni kujipotezea heshima. Wanachohitaji ni kutamkwa midomoni mwa wengi hata kama ni kwa jambo baya.

Skendo zao zimekuwa ni za aina mbalimbali. Lakini nyingi zaidi zimekuwa ni zile zinazogusa hisia za kingono.

Zikiwa zimebaki siku chache kuuaga mwaka 2018 na ku

ingia 2019, Gazeti la Risasi linalotoka kila Jumatano na Jumamosi linakuletea ‘Top Ten’ ya zile skendo za mastaa zilizotikisha zaidi kwa mwaka 2018;

 

DIAMOND NA ZARI

Februari 14, 2018 (Valentine’s Day) itabaki kwenye rekodi kuwa jamaa anayefanya poa zaidi kwenye Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alitemwa rasmi na aliyekuwa baby-mama wa watoto wake wawili, Tiffah na Nillan, Mganda Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

 

Zari alifikia hatua hiyo ya kutapika nyongo kwa kile alichodai kuwa alikuwa amechoka kuvunjiwa heshima kwa muda mrefu na mzazi mwenzake huyo hivyo akaona bora akae pembeni kuepusha msongamano na kilichobaki ni kuwalea tu watoto wao hao wawili.

Hata hivyo, Zari ambaye Diamond alimwachia nyumba huko Afrika Kusini hajaweka wazi kama ana mwanaume mwingine, tofauti na Diamond ambaye ‘amepita’ na wengine na sasa yupo kwa mtangazaji wa nchini Kenya, Tanasha Donna.

Gigy Money

DIAMOND NA HAMISA

Miongoni mwa mambo yanayoelezwa kumchosha kabisa Zari na kuamua kuchukua hamsini zake kwa Diamond

ni ile skendo matata iliyotikisa ya jamaa huyo kuthibitika kuzaa na mwanamitindo wa Kibongo, Hamisa Mobeto.

Wakati Diamond akiwa kwenye mkwaruzano na Zari, aliibuka Hamisa na kuthibitisha kuzaa na Diamond mtoto wa kiume aitwaye Dylan.

 

Hata hivyo, baada ya ishu hiyo kubumburuka, Diamond hakuendelea na Hamisa kwani ilifikia hatua mrembo huyo akamfikisha mahakamani kwa ajili ya matunzo ya moto ambapo staa huyo alikubali kufanya hivyo.

DIAMOND NA TUNDA

Wakati mambo yakiwa moto, iliibuka skendo nyingine ya Diamond kudaiwa kumtundika kibendi video queen wa Ngoma ya Chambua Kama Karanga, Tunda Sebastian.

Tunda au Kitoto Ndizi Maini alithibitisha kuwa na mimba ambayo alikataa katakata kuwa siyo ya Diamond.

Hata hivyo, baadaye ilisemekana mimba hiyo iliyeyuka huku Diamond akishangaa kuambiwa ‘mzigo’ huo ulikuwa wa kwake.

 

NANDY NA BILNAS

Miongoni mwa skendo matata kwa 2018 huwezi kuacha ile ya wasanii wa Bongo Fleva, Nandy au The African Princes na Bilnas au Bilinenga kufuatia kuvuja kwa video yao chafu wakiwa chumbani kingono.

Katika sekeseko hilo, wawili hao ambao awali walikuwa wakikanusha kuwa wapenzi waliumbuka na ukweli ulijulikana.

 

Ili kuweka mambo sawa huku akitoka kwenye familia iliyoshika dini, Nandy alilazimika kuomba radhi kwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na Watanzania kwa jumla kisha ilisemekana ndiyo chanzo cha wawili hao kumwagana jumlajumla.

 

ESMA NA PETIT MAN

Mwaka 2018, bundi alitua kwenye ndoa ya dada wa Diamond ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii (socialite), Esma Khan na mumewe, Petit Man ambapo uzi ulioishikilia ulikatika.

Nyuma ya tukio la kuvunjika kwa ndoa hiyo kulitajwa mambo mengine zikiwepo tuhuma za uchepukaji na Petit Man ambaye ni mejeja wa wasanii wa Bongo Fleva kutokubalika kwenye familia ya kina Diamond.

Kwa sasa kila mmoja yupo na hamsini zake, lakini bado hawajawaanika wapenzi wao wapya.

UWOYA NA DOGO JANJA

Unaikumbuka ile ndoa iliyozua viulizo vingi mwaka jana ya staa wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya au Mama Krish na msanii wa Bongo Fleva

kutoka R Chuga, Dogo Janja?

Basi taarifa ikufikie kuwa yale yaliyotabiriwa na wengi baada ya kuwa wamepishana umri vya kutosha, mwaka 2018 yalitimia kwani nayo iliota mbawa.

Kuna mambo mengi yaliyosemwa. Ukiacha ishu ya umri ambapo Uwoya ni mkubwa kwa Dogo Janja, pia kulikuwa na mambo ya michepuko kwa wote.

 

Ilifika wakati Dogo Janja akadaiwa kutafutiwa mtaalam wa saikolojia ili kumweka sawa kutokana na penzi lake na Uwoya kwani ilisemekana alifikia hatua ya kukaribia kuwehuka.

Kwa sasa kila mmoja yupo na hamsini zake huku Uwoya akihusishwa na kigogo mmoja, lakini Dogo Janja bado hajakaa sawa.

 

WEMA NA PCK

Kwenye skendo, kila mwaka lazima staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu aache au kuweka rekodi. Ndivyo ilivyotokea 2018 kwani kwa mara nyingine alitengeneza vichwa vya habari baada ya kuvuja picha na video zake chafu akiwa kingono na jamaa aitwaye Patrick Christopher ‘PCK’.

 

Katika ishu hiyo ambayo Wema ana kesi yake kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, ilibidi aombe radhi kwa kitendo hicho, lakini haikusaidia kwani kesi ilibaki palepale huku mwanaume huyo ambaye inasemekana ni raia wa Burundi akiingia mitini hivyo naye anasakwa na Polisi.

 

AMBER RUTTY NA BWANA’KE

Wakati anakumbwa na skendo ya ulawiti, wengi tulijiuliza Amber Rutty ni nani? Ilifahamika kuwa ni msanii ambaye bado hajatoa ngoma yoyote, lakini alipata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na picha zake za utupu.

Ghafla Amber Rutty aligeuka maarufu kutokana video iliyovuja akiwa na bwana’ke, Said Mtopali ikiwaonesha wakifanya mapenzi kinyume na maumbile.

 

Baada ya kusambaa kwa video hiyo huku vijana wakirushiana kwenye simu, Amber Rutty na bwana’ke huyo walitakiwa kujisalimisha Polisi kisha walifunguliwa kesi inayoendelea kwenye Mahakama ya Kisutu huku wenyewe wakiachiwa huru kwa dhamana baada ya kusota mahabusu katika Gereza la Segerea.

 

SISTER FEY NA KIBEN’TEN

Baada ya kupotea kwenye ulimwengu wa wasanii wa Bongo Fleva, mwaka huu Sister Fey aliibuka na mwanaume aliyemzidi umri (kiben’ten) aitwaye Holly Star ambaye naye ni chipukizi wa Bongo Fleva.

Katika kutafuta ‘nitoke vipi’, basi wakawa wanajiachia tu mitandaoni kwa video za kingono, jambo lililosababisha wakamatwe na Polisi kisha kunyang’anywa simu zao.

 

Wawili hao walipewa sharti la kutotupia tena video na picha zao chafu mitandaoni huku Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akiwapa onyo kali.

Kwa hasira, wawili hao waliamua kufunga ndoa.

 

GIGY MONEY NA MOJ

Achilia mbali zile picha zake za utupu mitandaoni, lakini mwaka huu msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ alimwagana na mzazi mwenzake mtangazaji MO J aliyezaa naye mtoto wa kike aitwaye Maira.

Yapo mengi yanayodaiwa kuchangia kumwagana ikiwemo kutotulia kwa Gigy na mwanaume huyo kutokuwa na uwezo wa ‘kumkotroo’ mwanadada huyo mwenye vitimbi kila kukicha ikiwemo kujiachia na wanaume wengine.

WENGINE

Wapo wengine waliokumbwa na skendo zilizozoeleka za picha za utupu kama Sanchi na Pretty Kind.

Pretty Kind alifikia hatua ya kufungiwa kutojihusisha na kazi za sanaa kwa muda wa miezi sita huku Sanchi akiitwa na Waziri Shonza kwa ajili ya kuonywa, lakini hakwenda

Loading...

Toa comment