The House of Favourite Newspapers

TOT vs E.Africa Taarab Valentine’s Day… Kopa: Nitawaonesha Taraab ilivyo, Dar Live

STORI: AMANI | SHOW BIZ – EXTRA

KATIKA kuelekea Sikukuu ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa amewaambia mashabiki wake wajitokeze kwa wingi siku hiyo ambayo ni Februari 14, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar kwani atawaonesha mashabiki wake Taarab ilivyo.

ITAKUWAJE?

Akizungumza na Showbiz Xtra, Kopa ambaye usiku huo atakuwa na kundi lake la TOT akichuana vilivyo na mkongwe mwenzake wa Kundi la East Africa Melody alisema, anajua mashabiki wengi siku hizi wanapenda kuwasikia wakongwe kuliko wasanii wanaoibuka hivyo atatumia nafasi hiyo kuwapa ladha ya kitofauti.

“Sipendi niongee sana, kikubwa tukutane Valentine’s Day pale Dar Live ili niwape ladha iliyokamilika ya Taarab,” alisema Kopa.

Msikie naye Bi Mwanahawa

Bi Mwanahawa alisema hatawaangusha mashabiki wake kwani wamejiandaa vya kutosha.

“Kwa wale wasiojua maana kamili ya mirindimo ya Pwani basi wajisogeze ndani ya Dar Live kwani ni zaidi ya kutoana jasho usiku huo,” alisema Bi Mwanahawa.

ZITAKAZORINDIMA SASA

Akizungumzia shoo nzima, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa, usiku huo vibao vingi vitarindima ambapo kwa upande wa Khadija Kopa atashusha vibao vyake vyote vilivyowahi kubamba na ambavyo vinaendelea kubamba.

“Kopa ataanza na Mjini Chuo Kikuu, Fahari ya Mwanamke, Nimpe Nani, Kadandie, Magumegume na nyingine nyingi huku Bi Mwanahawa akirudisha mashambulizi kwa vibao vikali kama Wakerekwao, Wema na Roho Mbaya Haijengi,” alimaliza Mbizo.

SAPRAIZI KIBAO KUTOLEWA

Mbizo alimalizia pia kwa kapo 100 wa kwanza watakaopendeza watapata sapraizi kibao zilizoandaliwa na ukumbi huo sambamba na huduma bora ya VIP.

“Siku zote Dar Live huwa tunajali mashabiki wote wa burudani. Mbali na uwepo wa nyama choma, flat screen kila engo na red carpet safi ndani, usiku huo utakuwa wa kipekee kwa kuwapa kipaumbele kapo 100 wa kwanza watakaotoka chicha zawadi na pia huduma bora ya VIP.

“Wapendanao wote niwatoe pia wasiwasi, safu ya ulinzi imepangwa vizuri kwahiyo si jambo la kuhofia,” alisema Mbizo.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

 

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.