ROLLERS 0-1 YANGA, LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Dak ya 90, dakika nne zimeongezwa na mwamuzi.
Dak ya 88, Yanga wanafanya shambulio jingine, kipa Rollers anadaka na kupiga mbele.
Dak ya 85, zimesalia dakika tano pekee mpira umalizike, Yanga wamefanya mabadiliko, ametoka Balinya na Rafael Daudi amechukua nafasi yake.

Dak 82, mwamuzi amesimamisha saa yake ya mkononi, kipa Mnata amelala chini, wakati huo Rollers wanafanya mabadiliko.

Dak ya 81, Kona nyingine kuelekezwa Yanga, Rollers wanapambana
Dak ya 80, Rollers wanapata shambulizi zuri lakini linakosa umakini na mpira unatoka nje

Dak ya 76, Moro anaokoa mpira uliokuwa unaingia langoni mwa Yanga, maridadi kabisa.
Dak ya 75, Rollers wanapata kona nyingine.

Dak ya 74, mpira unarushwa kuelekea Rollers, wakati huo Rollers wanafanya mabadiliko.
Dak ya 73, Ally Sonso anarusha mpira baada ya Rollers kuutoa nje.
Dak ya 72, Toto amechukua dakika mbili tu anacheza faulo, mpira unaelekezwa kwenda lango la Yanga.
Dak ya 70, Yanga wanafanyiwa shambulio lingine tena na inakuwa kona.
Dak ya 69, mabadiliko kwa Yanga, Banka anatolewa na Toto anachukua nafasi yake. Kona imepigwa sasa, Yanga wanaokoa.

Dak ya 68, hatari katika lango la Yanga huku, ni kona
Dak ya 64, piga pale, anakosaaa, kpa wa Yanga anadaka vizuuri kabisa mpira

Dak ya 62, kadi ya njano inaenda kwa mchezaji wa Yanga, ni Tshishimbi, na mwamuzi anatoa penati.
Dak ya 61, mpira unarushwa tena kuelekezwa Rollers, ni karibu na goli lao.
Dak ya 61, hatari katika lango la Rollers, beki yao inaokoa mashambulizi
Dak ya 60, Mo Banka amekuwa hana kiwango kizuri leo, anashindwa kutumia pasi za wenzake vizuri.

Dak ya 57, tayari Yanga wameshaanza kujivuta mdogomdogo wakiwa hawana haraka, na mpira wanarusha kuelekeza Rollers.

Da ya 53, Offside, Yanga wanaotea na mpira unapigwa kuelekezwa langoni kwao.
Dak ya 52, Yanga wameonekana kuamka, wamekuwa wakionesha mashambulizi mara nyingi.
Dak ya 48, kipindi cha pili kimeshaanza, matokeo bado Yanga inaongoza 1-0

HALF TIME: Yanga inaenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0
Dak ya 47, muda wowote mpira unaenda mapumziko

Dak ya 40, Pigwa kule gooooooli, Balinya anapiga bonge la faulo na kumuacha kipa wa Rollers akiwa hana pa kwenda, sasa ni 1-0
Dak ya 39, Faulo, Yanga wanapata faulo pia nje kidogo ya 18, kama wakitulia hapa wanaweza kuandika bao la kuongoza

Dak ya 36, wanakwenda sasa Rollers wakiishambulia Yanga, piga mbele kule, safu ya ulinzi ya Yanga inakuwa imara.
Dak ya 32, Uwanja wa Rollers hauna wengi, ni wachache waliopo.
Dak ya 31, Yondani anaonesha uzoefu kwa kuokoa baadhi ya mipira kutoka kwa washambuliaji wa Rollers.

Dak ya 30, Rollers wanakwenda, pigwa shuti gu la kushoto langoni mwa Yanga lakini mpira unakuwa juu ya lango.
Dak ya 29, Balama na mpira sasa, pasia kati ya uwanja lakini Rollers wanauchukua.

Dak ya 28, Boxer anapata kadi ya njano baada ya kucheza madhambi.
Dak ya 26, Rollers wanapata kona nyingine hapa, inapigwa lakini inaokolewa.
Dak 24, milango bado ni migumu kwa pane zote mbili, kila timu inapambana kupata ushindi.

Dak 24, milango bado ni migumu kwa pane zote mbili, kila timu inapambana kupata ushindi.
Dak ya 21, Balamaaaa, piga shuti kali huku mbele lakini linapaa sentimita kadhaa juu ya lango la Rollers, inaonesha Yanga wameanza kuchachamaa.
Dak ya 20, Bado mechi haina makali ambayo wengi wametarajia, kila timu inasaka nafasi ya kupata bao.

Dak ya 18, Yanga wanapata kona, pigwa huku Sandney Urikhob anapiga kichwa lakini unapaa juu ya lango
Dak ya 15, Rollers wanaenda sasa eneo la kati mwa uwanja, mabeki Yanga wanaokoa na sasa wanaanza kusaka upenyo wa kwenda mbele
Dak ya 15, Yondani anapiga shuti moja mbele, linapoteza mwelekeo na Rollers wanaokoa
Dak ya 13, Yanga wanarusha mpira, Boxer anaenda kurusha kuelekea Rollers
Dak ya 12, Bado washambuliaji wa Yanga kama Balinya, Bigirimana hawajaonesha makali uwanjani

Dak ya 11, Rollers wanapata kona ya kwanza, inapigwa lakini inaokolewa na mabeki wa Yanga
Dak ya 8, Yanga wanapata kona ya kwanza, inapigwa lakini inashindwa kuzaa matunda
Dak ya 7, Paul Boxer anarusha mpira kuelekea lango la wapinzani
Dak ya 4, kosakosa imetokea katika lango la Township, Yanga wanakosa nafasi ya kupachika bao
Dak ya 2, mechi imeshaanza huko Botswana kati ya Yanga na Township Rollers

CREDIT: GEORGE MGANGA | GPL


Loading...

Toa comment