The House of Favourite Newspapers

Toxstar Kuwaburuza Kortini Belle 9, G Nako

0

 

Staa wa ngoma ya Pretty Girl Toxstar.

STORI: Ally Katalambula | Uwazi | ShowBiz

Staa wa ngoma ya Pretty Girl ambaye wimbo wake wa Chillux aliomshirikisha Barnaba ndiyo habari ya mjini kwa sasa amesema kuwa anafikiria kwenda kortini kuwashitaki wanamuziki wenzake Belle 9 na G Nako kwa kutumia wazo la ngoma yake ya Ole ambayo aliitoa mwaka 2014.

Staa wa Bongo Fleva, Belle 9.

Akizungumza na safu hii ya burudani, Toxstar alisema wimbo huo uitwao ‘Ole’ alioutoa mwaka 2014 na wa Belle 9 uitwao ‘Mahole’ kila kitu kinaendana, jambo linalomshangaza ni wao kufanya hivyo bila kumshirikisha kwa lolote lile.

“Kiukweli siwezi kukubali, wimbo wa Belle na G Nako wamekopi na kupesti kwenye wimbo wangu wa Mahole bila hata kunishirikisha, hili si jambo sawa na ninachokifikiria kwa sasa ni kuwapeleka wawili hawa kortini,” alisema Toxstar.

Leave A Reply