The House of Favourite Newspapers

TP Mazembe Yamtoa Singano Kwa Mkopo Nkana

0

KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefikia makubaliano ya kumtoa kwa mkopo wa mwaka mmoja mchezaji wa zamani wa Simba SC na Azam FC, Mtanzania Ramadhani Singano, kwenda Nkana FC ya Zambia.

 

Singano alijiunga na TP Mazembe pamoja na Eliud Ambokile lakini uwepo wa wachezaji mahiri lukuki katika klabu ya TP Mazembe kumemfanya kukosa nafasi ya kucheza, hivyo kuhatarisha viwango walivyokuwa navyo.

 

TP Mazembe pia inaarifiwa kuwatoa kwa mkopo Singano na Isaac Amoah kwenda Nkana FC ili wapate muda wa kucheza na kurejesha makali yao yaliyowashawishi bosi wa vigogo hao, Moïse Katumbi Chapwe, kufungua pochi yake kuwasajili.

Leave A Reply