Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma za kifedha kwenye Tawi la Benki ya Posta Babati mkoani Manyara leo Februari 9, 2016. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, na kushoto ni Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya.
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (wa pili kushoto), akimpa zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya Posta Tawi la Babati, Theofil Muhale Tsaghayo baada ya kufungua rasmi huduma za kibenki katika tawi hilo, mkoani Manyara Februari 9, 2016. kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Prof. Lettice Rutashobya.
Na Mwandishi wa K-VIS MEDIA, Babati
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imezindua huduma za Kibenki kwa kufungua tawi lake jipya kwenye Mji wa Babati mkoani Manyara.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Februari 9, 2016, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Lettice Rutashobya alisema
tawi lililokuwepo hapo awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji wa Babati na vitongoji vyake kutokana na udogo wake.
tawi lililokuwepo hapo awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji wa Babati na vitongoji vyake kutokana na udogo wake.
‘’Tawi hili limefunguliwa ili kutimiza dhamira ya Benki yetu ya kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake, na sasa Tawi hili litatoa huduma bora na za kisasa ikiwemo ile ya ATM kwa wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika wilaya hii ya Babati”, aliwahakikishia Profesa Rutashobya.
Profesa Rutashobya pia aliwashukuru wateja wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma za Benki hiyo kwa wingi, na kulifanya tawi hilo kuwa ni mojawapo ya matawi yanayofanya vizuri kifaida.
Naye Msajili wa Hazina, Lawrence N. Mafuru, ambaye ndiye aliyezindua huduma za kibenki za tawi hilo, aliipongeza Benki ya Posta kwa kuleta maendeleo ya kuinua maisha ya Mtanzania ya hali ya chini kwa kuongeza huduma za kibenki karibu na jamii hiyo, na kwa kubuni huduma mbalimbali hususan za mikopo, zenye lengo la kumuinua kimapato mwananchi wa chini.
Msajili huyo wa hazina, alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wakazi wa Babati kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya Posta, kwa kufungua akaunti na kwenda kuomba mikopo ambayo inatolewa kwa riba nafuu na benki hiyo.
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru na maafisa wengine wakishangilia baada ya kukata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa huduma za kibenki katika tawi jipya la Benki ya Posta, Mjini Babati mkoa wa Manyara Jumanne Februari 9, 2016. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, (kulia) na Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi, Profesa Lettice Rutashobya.
Bodi ya Wakurugenzi, Profesa Lettice Rutashobya.
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Pamoja na Menejimenti ya benki hiyo, baada ya ufunguzi wa huduma za kibenki katika
tawi jipya la Babati, Manyara.
tawi jipya la Babati, Manyara.
Lawrence Mafuru (kushoto), akikabidhiwa kadi ya ATM ya benki ya Posta Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, baada ya kufungua akaunti muda mfupi baada ya kuzindua huduma za kifedha kwenye tawi la benki hiyo, mjini Bababati mkoani Manyara Feruari 9, 2016.