TRA Yaamuru Kuuzwa Magari Yaliyotelekezwa Bandarini – Video

KILA Jumamosi, ndinga mpya za bei chee zinaanikwa! Kampuni ya Udalali ya Tambaza Auction Mart and General Brockers Ltd iliyopewa idhini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kupiga mnada mali zilizotelekzwa bandarini na zile ambazo wateja wake wameshindwa kuzilipia kodi.

 

Wiki hii tambaza watakuwa na mnada mwingine mkubwa wa hadhara ukihusisha magari na vitu vingine kibao, utakaofanyika katika Bandari Kavu ya Dar es Salaam, Jumamosi hii, Julai 13, 2019.

 

Magari hayo ni yale yaliyoingizwa nchini kisha wenye nayo wakashindwa kuyalipia kodi hivyo yakataifishwa na Serikali kwa mujibu wa sheria hivyo yanauzwa katika mnada wa wazi baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.

 

Akizungumza na Global TV Online, Ofisa wa Tambaza Auction Mart, Sabrina Hamza amesema wananchi wote wanaruhusiwa kwenda kukagua bidhaa zote zitakazouzwa kwenye LCDs zilizopo ofisi za LW9, Bandarini, nyuma ya Police Central kuanzia kuanzia kesho Alhamisi ili siku ya mnada wanunue kirahisi.

 

 

Amesma baadhi ya vifaa vitakavyopigwa mnada Jumamosi ni pamoja na magari ya kisasa, vifaa vya kilimo, ujenzi nondo, tiles, mitumba na vitu kibao.

 

Mbali na hivyo, pia kutakuwa na kompyuta, viatu, mabegi, makontena ya nguo, ndondo, rangi za nyumba, mataili ya gari, baiskeli za watoto na vitu vingine kibao.

 

Mnada huo wa aina yake utaanza Jumamosi saa 4:00, Ubungo.

 

(Kwa Mawasiliano piga 0713 327 989 au 0715 683 777 au 0713 508 158 au nenda ofisini kwao, Sinza Mori ama jengo la RITA, Ghorofa ya 18, Posta Dar).

Website: tambazaauctionmart.com

TAZAMA VIDEO HAPA


Loading...

Toa comment