The House of Favourite Newspapers

TRA Yazuia Magari ya TFF Kuingia Ndani

IKIWA bado ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zikiwa zimefungwa kutokana na kudaiwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imebainika magari ya maofisa wa shirikisho hilo yamepigwa pini kuingia ndani.

Machi 15, mwaka huu, Kampuni ya Udalali na Minada ya Yono, ilitinga katika ofisi hizo zilizopo Ilala jijini Dar na kuwatoa nje wafanyakazi wote wa TFF na kuwataka waache kila kitu ndani.

Juzi Jumatano mchana, Championi Ijumaa lilitinga ofisini hapo na kukuta geti kubwa la kuingilia likiwa limefungwa na magari mengi yakiwa nje ya geti hilo huku kukiwa hakuna dalili za geti

kufunguliwa kwa siku za hivi karibuni.

Hivi karibuni iliripotiwa kwamba pande hizo mbili zipo kwenye mazungumzo ya kumaliza suala hilo, lakini hali inayoonekana bado hawajafikia makubaliano.

Alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas kutaka kuzungumzia hali hiyo, alijibu kwa kifupi kwamba bado ofisi zao hazijafunguliwa na hawajui ni lini zitafunguliwa.

Comments are closed.