The House of Favourite Newspapers
gunners X

 Trafiki anaswa kwa rushwa

0

trafikiJESHI la polisi mkoani Tanga limemnasa Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Koplo Antony Temu kwa kudaiwa kupokea rushwa.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, SACP Godfrey Kamwela alisema askari huyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi kutokana na kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii inayomuonesha akipokea fedha.

“Kutokana na video hiyo ndiyo maana tunamshikilia ili kufanya uchunguzi kama ni kweli alikuwa akipokea rushwa, baada ya uchunguzi ndipo tutakapojua kama alitenda kosa au la,” alisema Kamanda Kamwela.

Wiki hii kwenye mitandao kadhaa ya kijamii kuna video inamuonesha askari mmoja aliyedaiwa kuwa ni wa Kituo cha Polisi Kabuku akipokea burungutu la fedha na kuzisokomeza kwenye shati lake eneo la tumboni.

Katika mitandao hiyo, imedai kuwa askari huyo aliyevaliwa nguo za polisi wa usalama barabarani alikuwa akipokea mlungula.

Hata hivyo, haikujulikana mara moja watu waliokuwa wakimpa fedha hizo ambazo ni ‘nyekundunyekundu’.

Leave A Reply