The House of Favourite Newspapers
gunners X

TRC Yasitisha Safari za Treni ya SGR Kati ya Dodoma na Morogoro

0

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kusitisha safari za treni ya mwendokasi (SGR) kwa ruti ya Dodoma – Morogoro kwa muda kwanzia hii leo Disemba 31, 2025 kwa kile kilichotajwa uharibifi wa miundombinu uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli imeeleza “Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapenda kuutarifu Umma kusitishwa kwa safari za treni ya SGR kwa muda kuanzia tarehe 31 Disemba 2025 kati ya Morogoro – Dodoma na Dodoma – Morogoro kutokana na athari za mvua zilizopelekea uharibifu wa miundombinu katika eneo la Kidete (Kilosa, Morogoro) na Godegode (Mpwapwa, Dodoma).”

“Kufuatia athari hiyo, safari zote za SGR zitakuwa kati ya Dar es Salaam – Morogoro na Morogoro – Dar es salaam hadi pale marekebisho yatakapokamilika na usalama kuthibitishwa. Hivyo abiria wanashauriwa kubadili ratiba za safari zao kuendana na mabadiliko yaliyotokea.”

Leave A Reply