Treni iliyobeba tindikali yapata ajali

Queensland, Australia
Treni ya mizigo, iliyokuwa imebeba lita 200,000 za tindikali hatari ya Sulphuric Acid, usiku wa kuamkia leo Jumatatu imepata ajali nje kidogo ya Mji wa Julia Creek, Kaskazini Magharibi mwa Jimbo la Queensland nchini Australia na kuzua hali ya sintofahamu.

TreniPicha ya treni hiyo iliyopigwa kutokea angani

Polisi walilazimika kufunga shughuli zote zilizokuwa zikiendelea kwenye eneo la kilometa 2 kuzunguka eneo la ajali, wakihofia wananchi wanaweza kupata madhara makubwa kwa kugusa tindikali hiyo yenye tabia ya kuunguza ngozi ya mwili.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na shughuli za uokoaji zinaendelea ambapo wahudumu wawili waliokuwa ndani ya treni hiyo, wamejeruhiwa kwa tindikali na wanaendelea kupata matibabu.

Loading...

Toa comment