#GlobalCelebrityUpdates: Trevor Noah Sio Wa Mchezo Mchezo! Hii Ndio Nyumba Yake Mpya Ya USD $10 Million – (Pichaz)

Trevor Noah sio wa mchezo mchezo! Akiendelea kukitendea haki kipindi cha The Daily Show, haya ndio maisha anayoishi mchekeshaji huyo nchini Marekani kwa sasa.

Trevor Noah amenunua nyumba aina ya ‘Penthouse’ maeneo ya Midtown Manhattan nchini Marekani yenye thamani ya $10 Million ambayo kwa pesa ya hapa nyumbani ni zaidi ya shillingi Milioni 200 za Kitanzania. Kwa mujibu wa mtandao wa WSJ awali nyumba hiyo ilikuwa inauzwa kwa $11.5 million kabla ya bei kushuka.

Ndani ya nyumba hiyo kuna zaidi ya bafu 2 za kuoga na zaidi ya vyumba viwili vya kulala. Mtandao wa WSJ umeendelea kuripoti kuwa nyumba hiyo ni mfano halisi wa maisha anayostahili kuishi staa huyo.

Nimekuwekea hapa chini pichaz na video ya nyumba hiyo. Feel free kuipitia moja baada ya nyingine.

Mchekeshaji Trevor Noah mwenye asili ya South Africa ni miongoni mwa wachekeshaji wakubwa duniani na pia ni host wa kipindi kikubwa na maarufu cha comedy nchini Marekani ‘The Daily Show’ kinachoruka kupitia channel ya Comedy Central kwenye DSTV.

Itazame video ya nyumba mpya ya mchekeshaji Trevor Noah
hapa chini.

 

Source: WSJ

Imeandikwa Na: Sandra Brown.
Toa comment