The House of Favourite Newspapers

Trey Songz ataka kufanya kolabo na Davido

0

936full-trey-songzSTAA wa muziki wa R&B duniani, Trey Songz, kwa sasa yupo nchini Nigeria kwa ajili ya tamasha kubwa la muziki linalofanyika kila mwaka, Lagos, Nigeria lijulikanalo kama Pepsi Rhythm Unplugged 2015 na kuweka mikakati ya kutaka kufanya kolabo na staa wa muziki nchini humo, Davido.

davido-beardsTrey aliyasema hayo alipokuwa akitaka kupanda jukwaani kwa ajili ya kupiga shoo katika tamasha hilo ambapo alimwagia sifa Davido na kusema kuwa ni moja kati ya wasanii anaowakubali sana kwani ameweza kuubadilisha muziki wa Nigeria na kuwapagawisha wadada wengi kwa nyimbo zake.

Hata hivyo, Trey hajaweka wazi kolabo hiyo ataifanya lini.
Katika tamasha hilo lililofanyika huko Eko, Nigeria lilifunikwa pia na mastaa kibao wa Nigeria kama vile P-Square, Wizkid, Olamide, M.I., Korede Bello, Reekado Banks, Kiss Daniels, Runtown, Victoria Kimani, DJ Xclusive, DJ Cuppy na wengine kibao.

(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)

Leave A Reply