#GlobalCelebrities: Trey Songz Azungumzia Kuoa, Mapenzi na Nicki Minaj + Diss Track Ya Remmy Ma & Mengine Kwenye Beats 1 Radio – (Video)

Kwa wale wafuatiliaji wa muziki wa R&B superstaa Trey Songz, album yake ya saba Tremaine tayari imeshatoka na inagusa vitu muhimu vya maisha yake binafsi ikiwemo suala ya yeye kuoa na lini.

Trey Songz ameachia album yake ya saba iitwayo ‘Tremaine’ na kwa mujibu wa msanii huyo project hiyo mpya inagusa vitu vingi vya maisha yake binafsi ikiwemo suala la yeye kutulia kwenye mahusiano na mjadala wa lini ataoa. Kwenye interview aliyoifanya hivi karibuni na Beats 1 Radio, Trey amefunguka juu ya topic kubwa iliyobeba project yake mpya, lakini pia staa huyo ameongelea kwa ufupi uhusiano wake na Nicki Minaj pamoja na diss track ya Remmy Ma kwa Nicki Minaj.

Hivi ni baadhi ya vitu alivyovizungumza:

Kuhusu Album Yake Mpya ‘Tremaine’: 

Nimezungumza vitu vingi ambavyo ni personal kwenye hii album. Nimezungumzia pia familia yangu na jinsi ambavyo mama yangu anatamani na kuniuliza kila siku ntaoa lini na lini nitakuwa na watoto, je nahisi kama kuna uhitaji wa kuwa na familia kwa wakati huu… Sio kwamba nina haraka ya kufanya vitu vyote hivyo ila nimeongelea pia vitu ambavyo natamani ningekuwa navyo kwenye maisha yangu ya kimahusiano ambavyo nimeshindwa kuvitimiza…

Kuhusu watu wanavyochukulia maisha yake ya Kibachela:

Watu wengi wanafikiri kuwa kwa sababu tu nina uwezo wa kuwa na kumpata mwanamke yoyote yule nimtakaye basi ni rahisi kwa mimi kuoa, sio hivyo actually ni ngumu sana na jinsi maisha yangu yalivyo ya kusafiri safiri sana kiziara na vitu kama hivyo mara nyingi najikuta ni bora kuishi hivi, ila sio kwamba sitamani kuoa, bado sijaona mwanamke atakayeweza kuvumilia haya maisha… Kwahiyo nipo mguu moja ndani, mguu mmoja nje kwenye suala zima la kuoa ila natamani sana kutulia.

Kuhusu Nicki Minaj, na kama aliwahi kuwa naye kimapenzi kama Remmy Ma alivyodai:

Kama ningetaka kufanya kitu chochote na Nicki au kufeki mahusiano au mapenzi na Nicki ningekuwa nimeshafanya hivyo kitambo sana, kuanzia kipindi kile tunashoot music videos pamoja na kwenda kwenye tours pamoja, ila mimi sio wa hivyo nampenda na kumuheshimu Nicki ila bado kanikasirikia na sielewi kwa nini. Nimetembea na wanawake wengi sana lakini sijawahi kusema wala kuwasema kivyovyote kwenye mitandao, mimi sio mtu anayetumia kiki za mahusiano kujitengenezea njia za mafanikio. Nimefanya kazi nyingi na Nicki na nina muheshimu sana.

Kuhusu diss track ya Remmy Ma kwa Nicki Minaj:

Nadhani diss track ya Remmy Ma ilikuwa ngoma poa sana. Hii ni Hip Hop na kama shabiki niliona diss track ya Remmy ilikuwa imeshiba zaidi, aliweza kuchana na kufikisha kile alichotaka vizuri japo sikutegemea kama angenishambulia kama alivyonishambulia. Sasa matokeo yake na Nicki naye ananikasirikia… Ahahahaa!” 

Icheki interview nzima ya Trey Songz na Ebro Darden kwenye Beats 1 Radio hapa chini.

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Source: YouTube/Beats 1 Radio.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment