The House of Favourite Newspapers

TRIO 50KW: Mtambo Mpya wa Umeme wa Jua Kutoka ABB

UMEME wa jua umekuwa ukisaidia watu wengi si viwandani, ofisini bali hadi kwenye sekta binafsi. Wiki mbili zilizopita, nilihudhuria maonesho makubwa ya teknolojia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sandton Convention Centre jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

 

Kampuni ya uzalishaji na uuzaji wa vifaa vikubwa vya umeme ya ASEA Brown Boveri (ABB) kupitia kitengo cha umeme wa jua, walikuwa wakizindua bidhaa zao, ikiwemo mtambo mpya wa umeme wa jua unaotambulika kama Trio 50kW.

 

IPOJE HII?

Akizungumza ndani ya maonesho hayo katika mada ya kutoka Jua kwenda kwenye Soketi, mmoja wa wawakilishi wa Umeme wa Jua wa ABB nchini Afrika Kusini, alisema kuwa, ABB Trio-50 imekuja kuleta mapinduzi ya umeme wa jua.

 

“Trio ni kifaa maalumu ambacho kinafanya maunganiko ya umeme wa jua na kifaa hiki kina njia tatu za kupitisha umeme. Uzuri mmojawapo wa Trio ni urahisi wake wa kuitumia na pia ina uwezo wa kumudu kwenye biashara kubwa, kwani kifaa hicho kina uwezo wa kuzalisha umeme hadi 30MW,” alisema Mbali na uwepo wa Trio 50kW, ABB pia wana bidhaa nyingine za umeme wa jua ambazo zilikuwa katika maonesho siku hiyo ambazo ni;

PRO 33KW

Ni aina nyingine ya umeme wa jua inayoweza kutumika kwenye viwanda na sekta binafsi. Aina hii kama ilivyo kwa Trio, ni rahisi kuiweka na kuanza kuitumia, pia ina sehemu ya umeme wa mwisho kwa njia ya DC ambapo inaingiza hadi Volti 1100. Aina ya umeme huu umewahi kufungwa jijini Shropshire, Uingereza katika shamba kubwa na kuweza kuzalisha 900MWh kwa mwaka.

 

PVI 10 KW

Hii nayo ni aina nyingine ya umeme wa jua ambayo huanzia kW 10 hadi 12.5.Uzuri wa hii PVI imetengenezwa na Swichi maalumu za DC, fusi pamoja na rimoti ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha inaongoza umeme. Pia ina njia tatu ambazo zinatoa umeme wa DC na AC.

Makala: Andrew Carlos aliyekuwa Afrika Kusini

Comments are closed.