Trump Agoma Kushiriki Kikao cha Kumchunguza

WAKILI wa Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Ikulu ya White House haitashiriki katika kikao cha uchunguzi kitakachofanyika bungeni Jumatano ijayo.

 

Wakili huyo, Pat Cipollone amesema hawatashiriki katika kikao hicho chenye lengo la kujadili uwezekano wa kupitisha kipengele cha kumfungulia mashtaka rais huyo.

 

Katika barua hiyo Cipollone ameeleza kuwa hawawezi kushiriki wakati mashahidi wakiwa bado hawajatambulishwa, na huku wakiamini kwamba rais hatatendewa haki.
Toa comment