The House of Favourite Newspapers

Trump Amtimua Mkuu wa Jeshi Kitengo cha Ulinzi wa Fukwe

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi Kitengo cha Ulinzi wa Fukwe, Linda Fagan

Rais Donald Trump amemtimua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi Kitengo cha Ulinzi wa Fukwe, Linda Fagan katika namna inayotajwa kuwa ya kikatili muda mfupi tu baada ya rais huyo mtata kuapishwa.

Inaelezwa kuwa Trump aliandika barua ya kumfuta kazi kigogo huyo lakini ikachelewa kumfikia mhusika, ambapo akiwa kwenye hafla ya kijeshi iliyohudhuriwa na Trump, akiwa anasubiri kupiga naye picha ndipo alipofikishiwa barua hiyo na msaidizi wa Trump, Benjamine Huffman.

Gazeti la The New York Times limemnukuu afisa mmoja wa jeshi akieleza kuwa sababu zilizomfanya Trump ampige chini Fagan ni tuhuma za kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo ikiwemo kushindwa kudhibiti dawa za kulevya zinazoingizwa kimagendo kwa kupitia bahari sambamba na wahamiaji haramu wanaoingia Marekani kwa kupitia fukwe za nchi hiyo.

MTOTO ALIYETEKWA ALIVYOSHUSHWA KWENYE GARI na KUINGIZWA NDANI kwa SHANGWE – MAMA’AKE AZUNGUMZA…