The House of Favourite Newspapers

Trump Amwandikia Biden Ujumbe, Auacha Ikulu

0

ALIYEKUWA rais wa Marekani, Donald Trump, amefuata angalau utamaduni mmoja kama ilivyo kawaida kwa marais wanaoondoka madarakani.

Maafisa wa White House wanasema  Trump amemwandikia ujumbe Rais Joe Biden.

Naibu wa masuala ya habari katika White House, Judd Deere,  hajasema yaliyomo kwenye ujumbe wa Trump kwa Biden, akisema kwamba hizo ni kanuni za mawasiliano ya siri kati ya marais.

Trump amekataa kabisa kuutambua hadharani ushindi wa Joe Biden na wala hakutaja jina la Biden katika hotuba yake ya mwisho ya kuondoka madarakani.

Kiongozi huyo aliyepita amekosa kutimiza tamaduni za urais Marekani, ikiwemo kukataa kuhuduria sherehe ya kuapishwa kwa Joe Biden.

Aidha, hakumwalika Biden katika ikulu ya White House kwa mkutano kati ya rais anayeondoka na ayeingia madarakani, kama  ilivyo kawaida.

Leave A Reply