Trump Aondoa ushuru kwa simu za mkononi, kompyuta, na vifaa vingine vya kielektroniki
Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump, umeondoa ushuru kwa simu za mkononi, kompyuta, na vifaa vingine vya kielektroniki – hatua inayojumuisha pia kuondoa ushuru wa asilimia 125 uliokuwa ukitozwa kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani (US Customs and Border Protection), bidhaa hizo sasa zimeondolewa kwenye orodha ya ushuru wa asilimia 10 uliokuwa ukiathiri nchi nyingi duniani, pamoja na ule wa juu zaidi dhidi ya bidhaa kutoka China.
Rais Trump, akiwa njiani kuelekea Miami, ameahidi kutoa taarifa zaidi kuhusu hatua hiyo katika siku chache zijazo.