Trump Apatikana Na Kesi Ya Kujibu Kwa Kuchukua Nyaraka Za Siri Za Serikali Na Kupeleka Nyumbani Kwake
Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump amepatikana na kesi ya kujibu kuhusiana na katua yake ya kuchukua nyaraka za siri za serikali, alipokuwa anaondoka white house baadaa ya kushindwa katika uchaguzi mkuu.
Wataalam wa mahakama ya serikali kuu katika jimbo la Florida, wamempata Trump na makosa hayo na kumfanya kuwa aliyekuwa rais wa kwanza wa Marekani kufunguliwa makosa katika mahakama ya serikali kuu.
Trump ankabiliwa na mashtaka saba, ambayo hayajatangazwa wazi, ikiwemo kuvunja sheria za serikali kuu zinazozuia mtu yeyeote kuchukua nyaraka za serikali zinazohusu usalama wa taifa, kosa ambalo lina hukumu ya miaka 10 gerezani.
Trump ameandika kwenye ukurasa wa mtandao wake wa Truth social kwamba ametakiwa kufika mahakamani Miami, jumanne.
Maafisa wa FBI walipata sanduku kadhaa za nyaraka za siri za serikali, nyumbani kwake Trump, Florida, Agosti mwaka uliopita.