Trump: Atakayeshambulia Magari ya Tesla Atakiona – Video
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba vitendo vya fujo au uvamizi wowote kwenye ofisi za kampuni ya kuuza magari ya Tesla pamoja na matawi yake vitahesabiwa kuwa ‘ugaidi wa ndani,’ na wale watakaofanya hivyo watakiona cha mtema kuni.
Trump ameyasema hayo katika shoo maalum iliyofanyika Jumanne kumuunga mkono swahiba wake, Elon Musk, ambaye ndiye mgunduzi wa magari hayo ya umeme. Aliongeza kuwa na yeye atanunua gari moja ili kuonesha mfano kwa Wamarekani.
Wanaharakati nchini Marekani wanahamasisha maandamano na kugomea magari ya Tesla kama njia ya kupinga hatua za Elon Musk kupitia Idara ya Ufanisi Serikalini, aliyopewa na Trump, kushauri upunguzaji mkubwa wa wafanyakazi na kusitishwa kwa misaada ya kibinadamu.