The House of Favourite Newspapers

Trump Atoa Amri Jeshi Liwapige Magaidi wa Islamic State

Rais wa Marekani, Donald Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa ni yeye aliyeidhinisha mashambulizi ya anga ya Jeshi la Marekani nchini Somalia jana, Jumamosi, Februari 1, 2025, yaliyolenga magaidi wa Islamic State, ambao alisema walikuwa wakipanga shambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake.

“Hawa wauaji, ambao tumewakuta wakiwa wamejificha kwenye mapango, walikuwa wanaitishia Marekani na washirika wake,” aliandika Trump kupitia Mtandao wa Kijamii wa Truth.

“Mashambulizi yameharibu mapango yao walimokuwa wakiishi, na kuwaua magaidi wengi bila kuwaathiri raia kwa namna yoyote,” aliandika.

Mashambulizi ya jana Jumamosi yaliilenga milima ya Golis, yaliko maficho ya IS, huku Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, akiliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa hakuna raia aliyedhurika.

ZAHARANI MKUU wa SHULE AJIUA kwa SUMU SHINYANGA – ALIKIMBIZWA HOSPITALI AKAFARIKI AKIPATIWA MATIBABU