The House of Favourite Newspapers

Trump Atoa Pole Kwa Wafiwa 26 Waliouawa Kanisani Texas (Live Video)

0
Rais wa Marekani, Donald Trump.

RAIS Donald Trump wa Marekani ametoa pole kwa wafiwa wa watu 26 waliouawa kwa kupigwa risasi na mtu mwenye silaha katika kanisa moja jimbo la Texas wakati wa ibada, maofisa wanasema.  Shambulio hilo lilifanywa katika kanisa la First Baptist Church katika mji wa Sutherland Springs, mji mdogo katika wilaya ya Wilson, Texas.

Mshambuliaji, ambaye anadaiwa kuuawa baada ya kufanya mauaji hayo, aliingia kanisani na kuanza kufyatua risasi saa tano na nusu asubuhi (17:30 GMT).

Gavana Greg Abbott amethibitisha kufariki kwa watu haoakisema ni tukio baya zaidi lililowahi kufanywa kwa kutumia bunduki katika historia ya jimbo hilo.

“Kutakuwa na majonzi na masikitiko mengi kwa wale walioathiriwa,” Abbot aliwaambia wanahabari.

Mkuu wa idara ya usalama wa Texas, Freeman Martin, amesema waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka mitano  na 72.  Pia inasemekana watu zaidi ya 20 pia walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini.

Martin amesema mshukiwa ni mwanamume Mzungu mwenye wa umri wa miaka 20 ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi na fulana ya kujikinga dhidi ya risasi  na akiwa na bunduki mkubwa.  Alianza kufyatua risasi nje ya kanisa kabla ya kuingia ndani na kuendelea kufyatulia watu risasi.

Mshukiwa huyo anasemekana aliliangusha katika barabara wilaya ya Guadaloupe.  Polisi walimpata mshukiwa akiwa amefariki ndani ya gari lake.

Haijabainika iwapo alifariki kutokana na majeraha ya risasi aliyojisababishia mwenyewe au kutokana na mejaraha kutoka kwa raia huyo, Martin ameongeza.  Mshukiwa ametambulikana kuwa Devin P Kelley, 26, kwa mujibu wa vyombo vya habari Marekani.  Polisi bado hawajathibitisha jina lake.

Mhubiri wa kanisa hilo la First Baptist, Frank Pomeroy, ameaimbia ABC News kwamba binti yake wa miaka 14 aitwaye Annabelle ni miongoni mwa waliouawa.  Sutherland Springs ni mtaa mdogo wenye wakazi wasiozidi elfu moja ambao hupatikana kilomita 50 hivi kusini-mashariki mwa mji wa San Antonio mjini Texas.

Maofisa wa FBI kutoka San Antonio wametumwa kufanya uchunguzi lakini kufikia sasa lengo la mshambuliaji halijabainika.

Mauaji hayo yametokea mwezi mmoja tu baada ya mshambuliaji mwingine kuwafyatulia risasi watu waliokuwa katika tamasha la muziki Las Vegas na kuwaua watu 58 na kujeruhi mamia wengine.

Leave A Reply