Trump Awaka Kupekuliwa na FBI, Adai ni Njama za Kumrudisha Nyuma Kisiasa

FBI wakikagua makazi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

FBI ilipekua makazi ya Donald Trump ya Mar-a-Lago kama sehemu ya uchunguzi wa kama alichukua nyaraka za siri kutoka Ikulu ya WhiteHouse na kupeleka kwenye makazi yake hayo huko Florida nchini Marekani.

 

FBI Wamekataa kusema kama wamepata chochote baada ya ukaguzi huo, Familia ya Trump inasema kuna ajenda ya kisiasa nyuma ya uvamizi huo wa FBI kudhoofisha nia yake ya kugombea tena urais.

Trump amesema kinachofanyika ni harakati za kumrudisha nyuma kisiasa

Mbali na hilo, pia Trump amejikuta kwenye matatizo na shutma za kuchochea vurugu na maandamano pamoja na matumizi mabaya ya madaraka wakati wa utawala wake kwa kuweka watu wasio na sifa kwenye nafasi za utawala.

 

Ofisi ya Trump ilitoa tamko lililosema:

 

” Tukio kama hili halijawahi kumtokea kwa Rais yeyote wa Marekeni. Baada ya kushirikiana na taasisi za serikali tumeona kwamba, uvamizi huu haukuwa sawa.”

Moja ya makazi ya Donald Trump

“Haya ni makosa ya kisheria, matumizi mabaya ya nguvu kwenye mifumo ya utoaji haki na ni njama za wanasiasa wengine dhidi yangu wasiotaka niwanie tena nafasi ya Uraisi mwaka 2024.”

 

Wachambuzi wa mambo ya sheria wamesema uvamizi huo hauonekani kama ulikusudia kushusha heshima ya Rais huyo ili kudhoofisha malengo yake ya kugombea mwaka 2024, bali ulilenga kupata nyaraka za muhimu zilizodhaniwa kuchukuliwa na Raisi huyo wa zamani wa Marekani kwa manufaa mapana ya taifa la Marekani.

Imeandikwa: Abdallah Ally kwa msaada wa mitandao

4229
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment