The House of Favourite Newspapers

Trump: Kanye West Anaweza Kuwa Rais!

0

HARAKATI za mwanamuziki Kanye West wa Marekani kutaka kuwa Rais wa nchi hiyo zilianza siku nyingi kabla ya wikiendi iliyopita kutangaza rasmi kugombea mwaka huu.

 

Kwa miaka kadhaa Kanye West amekuwa akizungumzia suala la kuwania urais nchini Marekani ambapo siku moja Rais wa sasa, Donald Trump aliulizwa kama anaweza, akajibu; “Sana tu anaweza kuwa!”

Baadhi ya watu wamekuwa wakimtilia shaka kuwa huwenda anatania au anatafuta kiki, lakini mwenyewe amesisitiza; “’Lazima sasa tutambue ahadi ya Marekani kwa kumuamini Mungu, kuunganisha maono yetu na kujenga mustakabali wetu.” Sasa imebaki miezi minne tu kabla ya uchaguzi nchini humo utakaofanyika Novemba 3, mwaka huu.

 

Yeye na mkewe, Kim Kardshian, wamefanya kazi na Rais Trump mara kadhaa ikiwemo wakati wa shughuli za kuwafungulia wafungwa.

Kanye West na mkewe waliwahi kumtembelea Trump kujadili mabadiliko katika magereza mwaka 2018.

STORI: NEW YORK, MAREKANI

Leave A Reply