The House of Favourite Newspapers

Trump Kung’olewa Madarakani?

0

Maprofesa watatu walioalikwa na Chama cha Democratic katika kikao cha kwanza cha kamati ya masuala ya sheria ya Baraza la Wawakilishi mjini Washington, wamesema tuhuma zilizotolewa dhidi ya Rais Donald Trump kuhusiana na Ukraine, zinakidhi vigezo vya kumfungulia mashtaka kiongozi huyo.

 

Kwa upande wa profesa wa nne aliyealikwa na Chama cha Republican, amesema ushahidi unaomhusisha Trump na vitendo vya kutafuta uingiliaji wa kigeni katika uchaguzi wa Marekani ni wa kusuasua, na hivyo hali hii inathibitisha mgawanyiko wa kisiasa nchini Marekani.

Leave A Reply