The House of Favourite Newspapers

Trump Uso kwa Uso na Rais Kagame, Atuma Salamu Afrika

Rais Trump (kushoto) akisalimiana na Rais Kagame.

RAIS wa Marekani, Donald Trump amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na kumuomba afikishe salamu zake za upenzo kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi baada ya Mkutano wa Viongozi na Watu Mashuhuri Kuhusu Uchumi na Biashara Duniani.

Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika.

 

Kutoka kusoto ni mama Jeannette Nyiramongi Kagame, Rais Kagame, Rais Trump na Melania Trump.

 

Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana ambapo amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyakashifu mataifa ya Afrika huku akikiri kutumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.

Wakati wa mkutano wake na Kagame,  Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika huku akisifia kuwa mkutano wao huo ulikuwa “wa kufana sana”, na kueleza nchi hizo mbili kama washirika wa kibiashara ambao wanajivunia “uhusiano mzuri sana.”

 

Trump akifanya mazungumzo na Kagame.

 

“Ningependa kukupongeza, Bw Rais, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa … najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza karibuni. Tafadhali, fikisha salamu zangu.”

Rais Kagame alisema wameshauriana kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Marekani kwa Rwanda katika operesheni zake kote duniani, pamoja na masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na idadi ya watalii wa Marekani wanaozuru Rwanda, ambayo inaongezeka. Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa AU utafanyika kesho Jumapili na Jumatatu.

 

NUSU UKWELI NUSU UTANI: UAMUZI WA JPM KWA MUHONGO UNAASHIRIA NINI KWA WATUMISHI?

Comments are closed.