Tshishimbi Aomba Kurejea Yanga

TAARIFA za ndani ya Klabu ya Yanga, zimeweka wazi kuwa, nahodha wa zamani wa timu hiyo, Papy Kabamba Tshishimbi, ameomba kurejea kuitumikia Yanga, kutokana na kuona bado anauwezo wa kuitumikia kwa mafanikio tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

 

Tshishimbi aliachana na Yanga mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na Klabu ya As Vita ya kwao DR Congo kwa mkataba wa mwaka mmoja.

 

Chanzo chetu kutoka ndani ya Yanga, kimenyetisha kuwa, kamati ya usajili inapitia maombi ya baadhi ya wachezaji ambao wameonyesha nia ya kujiunga nao msimu ujao akiwemo Tshishimbi.

 

“Kusema kweli kwa sasa kamati yetu ya usajili ipo kwenye mchakato mrefu wa kuangalia sifa za wachezaji tunaowahitaji ingawa kuna maombi mengi ya nyota wetu wa zamani kuomba kurejeatena akiwemo Tshishimbi ambaye aliondoka msimu uliopita.

 

“Tunaimani kama tukijiridhisha vizuri na maombi ya baadhi ya nyota hao waliomba nafasi ni dhahiri hakuna tutakayemkosa maana tunahitaji kutengeneza kikosi kilicho bora kwenye mashindano yote tutakayoshiriki msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.

 

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na ishu hiyo na mambo ya usajili yako kwenye kamati ya usajili.”Tecno


Toa comment