The House of Favourite Newspapers

Tshishimbi arejea mzigoni Yanga

shimbNYOTA Mkongo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi hatimaye amerejea rasmi ndani ya kikosi hicho juzi Jumanne na kuanza mazoezi baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.

Kiungo huyo alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambayo yalisababisha kukosa mechi zaidi ya tatu msimu huu kutokana na kutokuwa imara kiafya.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa Yanga, Hafidhi Salehe alisema kuwa mchezaji huyo ataendelea kufanya mazoezi ila mchezo wao na Reha uliopigwa jana Jumatano hakuwa ya wachezaji waliocheza kwa kuwa ndiyo kwanza ameanza mazoezi.

 

“Kurejea kwake ni jambo jema na la kheri kwa timu sababu anakuwa ameongeza nguvu hivyo hakuna tatizo mchezaji ambaye amesalia kwa sasa yupo nje ni Juma Mahadhi pekee,” valisema Hafidhi ambaye ni miongoni mwa watu waliodumu kwenye ofisi za Yanga zaidi ya miaka 10.

MARTHA MBOMA, DAR ES SALAAM

EXCLUSIVE : Bakili Makele wa Yanga Afunguka kufungiwa Kisa Manji

Comments are closed.